Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa 19 Chadema kizimbani kwa tuhuma za fujo kanisani
Habari za Siasa

19 Chadema kizimbani kwa tuhuma za fujo kanisani

Bendera ya Chadema
Spread the love

 

WANACHAMA 19 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), waliokamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, wakiwa kanisani, wamepandishwa kizimbani na kusomewa shtaka la kuleta usumbufu katika mkutano wa kidini. Anaripoti Mwanaharusi Abdallah, TUDARCo … (endelea).

Washtakiwa hao walisomewa shtaka hilo, leo Alhamisi, tarehe 19 Agosti 2021 katika Mahakama ya Mkoa wa Mwanza.

Wakili wa washtakiwa hao, Edward Heche amelieleza MwanaHALISI Online kwa njia ya simu.

“Ni kweli wamefikishwa mahakamani na kusomewa shtaka la kufanya fujo kanisani, hapa ninapozungumza tuko katika utaratibu wa kupata dhamana kwa kuwa kosa waliloshtakiwa dhamana yake iko wazi,” amesema Wakili Heche.

Wanachama hao akiwemo Katibu Mkuu wa Chadema Kanda ya Victoria, Zacharia Obad na wenzake 18, walikamatwa na Jeshi la Polisi, Jumapili ya tarehe 15 Agosti 2021, baada ya kushiriki ibada katika Kanisa Katoliki Parokia ya Kawekamo, jijini Mwanza.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema mkoani Mwanza, Boniface Nkobe, amesema wako katika jitihada za kukamilisha taratibu za udhamini, na kwamba washtakiwa hao watatoka leo.

“Kwa sasa tunahangaikia dhamana ya hiyo kesi, lakini hadi sasa bado hawajatamka rasmi mpaka lini watawarudisha mahakamani, lakini zoezi la kutafuta wadhamini linaenda vizuri, watatoka leo,” amesema Nkobe.

Mbali na Obad, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni, Eudia Frank, Yasinta Wachelele, James Mayala, Leah Paul Joseph, Michael Mtabuzi Christian, Dionise Edward, Elieza Petro Mkungu, Gadson Jacob.

Musa David Kimweli, Msafiri Jacksoni Nteminyanda, Frank Novatus Nyamuga, Emanule Mtani, David Benjamin Nyakimwe, John Mwita Nyamhanga, Farida Hamis Gilala.

Wengine ni, Deus Simon Shinengo, Mang’ombe Osward na Kelvin John.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo kinyume cha kifungu cha 126 cha Sheria ya Makosa ya Jinai.

Wanadaiwa kutenda kosa hilo tarehe 15 Agosti 2021, katika Kanisa Katoliki Parokia ya Kawekamo, wilayani Ilemela mkoa wa Mwanza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kamati ya Bunge yaitaka Serikali kuchunguza dawa za asili

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo...

Habari za Siasa

Kada NCCR-Mageuzi aliyepotea aokotwa porini akiwa taabani, hajitambua

Spread the love  MWENYEKITI wa Jumuiya ya Vijana ya Chama cha NCCR-Mageuzi,...

Habari za Siasa

ACT Wazalendo yataka Jaji Mkuu, Jaji Biswalo wajiuzulu kupisha uchunguzi fedha za Plea Bargaining

Spread the love  CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimemtaka Jaji wa Mkuu wa Tanzania,...

Habari za Siasa

Kigogo ACT-Wazalendo: Vyama vya upinzani vilikosea kumpokea Membe, Lowassa

Spread the love  KATIBU Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Ado Shaibu, amesema...

error: Content is protected !!