Monday , 26 February 2024
Home Kitengo Maisha Afya Tacaids watoa somo kwa wanahabari
Afya

Tacaids watoa somo kwa wanahabari

Spread the love

TUME ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) imeanza kutoa mafunzo kwa wanahabari wa vituo vya radio Jamii ili kuweza kusaidia kampeni ya kupambana na maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi. Anaripoti Dany Tibason … (endelea).

Jumanne Sango, kwa niaba ya mkurugenzi wa TACAIDS, amesema kuwa waandishi wa habari ni wadau wakubwa  na muhimu katika usambazaji wa habari kwenye jamii.

Amesema kutokana na umuhimu wao wameona ni vizuri kuwatumia ili kuweza kusaidia kuibua vichochezi vya maabukizi mapya ya ukimwi endapo watashirikishwa kikamilifu.

Sango amesema kuwa radio za kijamii zinapaswa kutambua changamoto zinazopatikana katika maeneo yao ili kuzitafutia ufumbuzi haraka kwa kushirikiana na TACAIDS.

“Kuna vichochezi vya maambukizi ya Virusi kulingana na mazingira japo kuna zile za jumla hivyo waandishi wa habari mnaweza kuziibua changamoto hizo,” amesema Sango.

Sango amesistiza kuwa ushiriki wa mwanaume katika kampeni ya kupima virusi vya ukimwi kwa hiari ni muhimu kwani ndio mihimili ya familia baada ya takwimu kuonesha kundi hilo kuwa nyuma.

“Mwanaume jali afya yako pima virusi vya ukimwi ndio kauli mbiu inayotumika katika kuwahamasisha wanaume kushiriki katika kampeni ya Furaha yangu ni kuona unaishi iliyozinduliwa na waziri mkuu, naombeni baada ya mafunzo haya tuwahamasishe wanaume kufika katika vituo vya afya na kupima afya zao,” amesema Sango.

Pia Sango amesema kuwa ni vema viongozi wa kisiasa wanaopewa madaraka na wananchi kutumia utashi wao katika kuhamasisha jamii juu ya upimaji wa VVU kwa hiari.

Naye ofisa uraghibishi na habari, Simon Kirago alieleza kuwa wanahabari ni wadau wakubwa katika jamii kwa kushirikiana na TACAIDS watasaidia kukomesha maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi na kutoa elimu kwa waathirika juu ya matumizi sahihi ya dawa za kupunguza nguvu (ARV).

Aidha aliongeza kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari katika kupambana na maambuki ya virusi na usamabazaji wa matokeo ya utafiti na viashiria vya Ukimwi uliofanyika nchi nzima.

TACAIDS inatarajia kufikia mwaka 2020 kufikia asilimia 903 zenye tafsiri ya asilimia 90 ya watanzania wawe wamepima virusi vya ukimwi, asilimia 90 wenye virusi vya ukimwi wawe wamejitambua na asilimia 90 wenye virusi wawe wameanza kutumia dozi ya ARV.

Richard Kalumuna moja kati ya washiriki wa mafunzo hayo alisema kuwa baada ya mafunzo wanategemea kuibadilisha jamii kwa kiwango kikubwa hasa kitengo cha ushauri nasaha ambapo panahitaji umakini wa hali ya juu kwa wale wanaokuwa tayari wameambukizwa.

“Sisi kama waandishi wa habari tutaendelea kutekeleza majukumu yetu ya kutoa taarifa kwa umma, kuelimisha umma na kwa kushirikiana na TACAIDS tutafanikisha katika hili,” amesema Kalumuna.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Dk. Biteko aagiza uboreshaji huduma za afya kwa wazee

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

AfyaTangulizi

Wanawake walalamikia ukubwa kondomu za kike, waomba zipunguzwe

Spread the loveWataalamu wa afya wilayani Ileje mkoani Songwe wameagizwa kuanza kutoa...

AfyaHabari Mchanganyiko

Madaktari wazawa watenganisha watoto mapacha walioungana

Spread the loveHospitali ya Taifa Muhimbili kwa mara nyingine imeandika historia kwa...

Afya

DC Mpanda aagiza maji ya visima yapimwe kudhibiti kipindupindu

Spread the loveMkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuf ameziagiza mamlaka za...

error: Content is protected !!