May 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wanafunzi UDSM waandamana

Spread the love

WANAFUNZI Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wameandamana usiku huu kutoka kampasi kuu ya Mlimani mpaka mabweni ya Mabibo, wakisherekea ushindi wa rais wao mpya. Anaripoti Charles William … (endelea).

Nhonya Haroun Stanley ndiye rais mteule wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, DARUSO ambapo amechaguliwa katika uchaguzi uliofanyika leo Jumatano chuoni hapo.

Haroun amewaangusha wapinzani wake Frank Isack na Matulanya Evarist katika uchaguzi uliojaa mvutano mkali huku Loveness Nkya akimuangusha Suzan Zabron katika nafasi ya makamu wa rais wao DARUSO.

Zaidi ya wanafunzi 5,000 walijitokeza kupiga kura.

error: Content is protected !!