December 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

167 mbaroni kwa tuhuma za kuvunja nyumba, kuiba

Spread the love

 

JESHI la Polisi nchini, limewakamata watu 167 kwa tuhuma mbalimbali, ikiwemo kuvunja nyumba za raia, kujeruhi na kuiba mali. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa Leo Jumamosi, tarehe 24 Septemba 2022, jijini Dar es Salaam na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, CP Awadhi Juma, akielezea matokeo ya operesheni maalum iliyofanywa na Polisi kuwakamata watu wanaojihusisha na vitendo hivyo vya kihalifu muda wa usiku wa manane, kwa kutumia silaha za jadi.

Amesema, kati ya watuhumiwa hao, wapo waliokamatwa kwa kosa la kununua mali zinazoibwa na vikundi vya kihalifu maarufu kama panya road.

CP Haji amesema watuhumiwa hao wamekamatwa katika nyakati tofauti Septemba 2022.

“Watuhumiwa hao wamegawanyika katika makundi, kundi la watuhumiwa wanaoshiriki moja kwa moja kuvunja nyumba, uporaji na kundi jingine linalopokea na kununua Mali hizo za wizi,” amesema CP Haji.

Aidha, CP Haji amesema watuhumiwa hao wamekamatwa wakiwa na mali mbalimbali za wizi, ikiwemo runinga za kisasa ‘Flat Tv’, redio na kompyuta.

error: Content is protected !!