May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

158,000 waomba ajira 17,000, Serikali yaongeza siku 4

Waziri wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Innocent Bashungwa

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania imeongeza siku nne zaidi kwa waombaji wa ajira za ualimu na afya kutoka jana Jumatano tarehe 4 hadi 8 Mei 2022, saa 5:59 usiku. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Innocent Bashungwa amesema hatua ya kuongeza siku hizo ni kutoa fursa kwa walioshindwa kuomba maombi hayo tangu zilipotangazwa 20 Mei 2022.

Amesema mpaka kufikia juzi Jumanne tarehe 3 Mei 2022 saa 5:59 usiku, waombaji waliowasilisha maombi kupitia mfumo wa kada ya afya ni 39,053 na kada ya elimu ni 119,133 hivyo jumla ya waombaji wote wakiwa 158,186.

Waziri Bashungwa amesema, Tamisemi ilipata kibali cha ajira za watumishi 9,800 kwa kada ya ualimu na 7,612 kwa kada ya afya ambapo ajira zote ni 17,412.

error: Content is protected !!