August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

156 wafukuzwa mafunzo ya Polisi kwa utovu wa nidhamu

Spread the love

 

INSPEKTA Jenerali wa Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro, amesema wanafunzi 156 wa Chuo cha Jeshi la Polisi, wamefukuzwa katika mafunzo ya awali ya kozi ya Askari Polisi, kwa makosa ya utovu wa nidhamu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

IFGP Sirro ametoa taarifa hiyo leo Jumanne, tarehe 29 Juni 2022, akizungumza na wanafunzi wa kozi ya awali ya Askari Polisi, katika Shule ya Polisi Tanzania, iliyopo mkoani Kilimanjaro.

“Toka mmekuja kuanza mafunzo, takwimu nilizo nazo takribani askari 156 wanafunzi wamefukuzwa jeshi kwa sababu ya utovu wa nidhamu. Kufanya mambo ambayo hayakubaliki ndani ya chuo cha Jeshi la Polisi,” amesema IGP Sirro.

Mkuu huyo wa Polisi, amewataka wanafunzi waliobaki kuwa na nidhamu ili wamalize masomo yao kwa kuwa familia zao zinawategemea.

“Mtambue sana kwamba Watanzania wanajua mko hapa na mategemeo yao mtarudi kwenda kuwasaidia kuhakikisha kunakuwa na utulivu, mnalinda mali zao na usalama wao. Familia zenu zinawategemea,”amesema IGP Sirro.

error: Content is protected !!