October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

150 mbaroni kwa makosa ya jinai

Jumanne Muliro, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam

Spread the love

 

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewatia mbaroni watuhumiwa zaidi ya 150 wa makosa ya jinai, 17 makosa ya unyang’anyi wa kutumia silaha  pamoja na pikipiki tatu ambazo zilikuwa zinatumiwa na wahalifu kwenye matukio hayo. Anaripoti Mwanaharusi Abdallah na Victoria Mwakisimba TUDARCo … (endelea).

Hayo yamejiria katika operesheni maalumu ya kuwatia mbaroni watuhumiwa wa makosa mbalimbali ya jinai ikiwa ni moja kati ya njia ya kuhakikisha jiji linakuwa shwari.

Akizungumza waandishi wa habari leo tarehe 16 Septemba, 2021, Kamanda mkuu kanda maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema operesheni hiyo ni endelevu.

Amesema kwa upande wa dawa za kulevya, jeshi hilo limekamata pakiti tano za heroine, kilogram 12 za bangi na kete 1005 za bangi.

Amesema katika maeneo ya Tegeta, Kitunda,  Kimara, Mbagala, Kivule na maeneo mbalimbali ya hapa jijini Dar es Salaam jumla ya watuhumiwa 97 wamekamatwa kwa makosa ya kufanya wizi majumbani nyakati za usiku na mchana.

error: Content is protected !!