May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Dk. Tulia ndio tatizo’

Dk. Tulia Ackson, Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Spread the love

DK. Tulia Ackson si mwanasiasa na ndio maana anayumbisha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anaandika Pendo Omary.

Ni kauli ya Mariam Msabaha, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Akizungumza na mwandishi wa habari hii leo mbunge huyo amefafanua kwamba, hatua hiyo inatokana na Dk. Tulia kukosa uzoefu.

Msabaha amesema, Dk. Tulia hatambui harakati za kuwawezesha wanawake kushiriki katika siasa sawa na wanaume.

Amesema, “wakati wa uongozi wa Spika Anna Makinda, wanawake walisikika sana. Makinda aliwajenga wanawake. Yeye mwenyewe (Makinda) amekulia kwenye siasa. Tangu akiwa binti mdogo.

“Hatua ya Makinda kutoa fursa kwa wanawake iliwahamasisha wanawake kugombea na kupata majimbo.

“Walikuwa wanajenga hoja, walikuwa na uhakika na bunge lilikuwa linakwenda ‘live’ na wanawake walipata nafasi,” amesema Mariam.

Mariam amesema, Makinda alikuwa akilisimamia Bunge akimchagua mwanaume aulize swali basi swali la nyongeza angempa nafasi mwanamke akauliza.

“Unaweza kukuta swali limeulizwa na mbunge mwanaume, na maswali ya nyongeza wanauliza wanaume.

“Ninachokiona katika bunge la sasa hivi ni kwamba, mwanamke unaweza kusimama hata fursa ya kuuliza swali la nyongeza hupati. Ni tofauti na bunge lililopita.

“Katika mabunge yote, sio tu Tanzania Spika au mbunge unapochaguliwa lazima upate semina elekezi. Dk. Tulia ni mwanasheria. Mambo yake ni ya kimahakama na sio mwanasiasa,” amesema Mariam.

error: Content is protected !!