Wednesday , 21 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ⁩ Samia aridhia Chongolo kujiuluzu
Habari za SiasaTangulizi

⁩ Samia aridhia Chongolo kujiuluzu

Spread the love

Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan leo Jumatano ameridhia kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Daniel Chongolo kutokana na barua aliyoiandika na kuielekeza kwa mwenyekiti huyo.  Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Uamuzi huo umetangazwa leo na Katibu wa NEC- Itikadi na Uenezi, Paul Makonda wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu yaliyojiri katika vikao vya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) vilivyofanyika jijini Dar es Salaam leo tarehe 29 Novemba 2023.

Makonda amesema nafasi hiyo ya Chongolo atakaimu Naibu Katibu Mkuu Bara, Annamringi Macha.

Katika vikao hivyo vilivyoanza jana Jumanne, gumzo lilikuwa yu wapi Chongolo… ambaye kutokana na umuhimu wa vikao hivyo huwa mmoja wa wajumbe au viongozi wanaoketi viti mbele kuongoza vikao hivyo.

Hata hivyo, katika baadhi ya picha hizo zilizosambaa katika mitandao ya kijamii jana na leo, Chongolo hakuonekana kushiriki vikao hivyo ambavyo leo vilikuwa vinaongozwa na Rais Samia.

Kabla ya taarifa ya Makonda tayari wadokezi wa siasa walikuwa wamesema wajumbe wa mkutano huo wamepokea barua hiyo ya Chongolo na kuiridhia kisha kuahidi kuwa uchunguzi wa tuhuma zinazodaiwa kumkabili kiongozi huyo, utachukua muda kukamilika.

Hata hivyo, wadokezi hao wanadai kuwa wajumbe wa mkutano huo wamempendekeza Naibu Katibu Mkuu (Tanzania Bara), Anamringi Macha kukaimu nafasi hiyo ya Chongolo hadi hapo taarifa ya uchunguzi itakapokamilika.

CHONGOLO ANATUHUMIWA NINI?

Kwa zaidi ya wiki sasa katika mitandao mbalimbali ya kijamii Chongolo anadaiwa kutumia madaraka yake vibaya kwa kuagiza kampuni moja ya bima kumlipa fidia ya gari yake ya kifahari aina ya Land Cruiser aliyopata nayo ajali.

Anadaiwa kuwa aliagiza kampuni ya bima kumlipa fidia ya matengenezo ya gari hilo ilihali halikuwa limekatiwa bima.

Pia anatuhumiwa kuwa mbali na ajali hiyo aliyodaiwa kupaita katikati ya mwaka huu, pia kumesambaa ujumbe mfupi (charting) unaoonesha alikuwa chart na mwanamke mwenye mahusiano naye ya kimapenzj huku wakitumiana picha za utupu.

Kabla ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo ya Katibu Mkuu tarehe 30 Aprili mwaka 2021, Chongolo alikuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni kuanzia mwama 2018.

Pia aliwahi kuwa mkuu wa wilaya ya Longido mkoani Arusha kuanzia mwaka 2016 nafasi ambazo aliteuliwa na Rais wa awamu ya Tano, Hayati John Magufuli.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Mwinyi ateua waziri wa uchumi na uwekezaji Zanzibar

Spread the loveRAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi,...

Habari za SiasaTangulizi

Mvua yakatisha mkutano wa Chadema Mbeya

Spread the loveMKUTANO wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),...

Habari za Siasa

Sugu atumia maandamano ya Chadema kumfikishia ujumbe Spika Tulia

Spread the loveALIYEKUWA Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi “Sugu”, ametumia maandamano...

Habari za SiasaTangulizi

Sakata la DP World na bandari lafufuka upya

Spread the loveSAKATA la mkataba wa kiserikali kati ya Tanzania na Imarati...

error: Content is protected !!