Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto: Mnazo sababu za kuing’oa CCM
Habari za Siasa

Zitto: Mnazo sababu za kuing’oa CCM

Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo
Spread the love

ZITTO Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo amewaeleza wanachama wa chama hicho Tunduru, Mtwara kwamba wanayo sababu ya kuing’oa CCM madarakani. Anaripoti Faki Sosi, Tunduru … (endelea).

Akizungumza kwenye mkutano wa ndani na wachama wa chama hicho tarehe 22 Julai 2020, Zitto aliye kwenye ziara ya kichama na baadhi ya viongozi wa chama hicho mkoani Mtwara amesema, safari hii ‘lazima kieleweke.’

Kwenye kikao hicho, Zitto amewapa mfano wa namna mikutano ya kisiasa ilivyozuiliwa huku akisitiza, Uhuru wa kujieleza miongoni mwa Watanzania umetoweka kutokana na hofu iliyojengwa na Serikali ya Awamu ya Tano.

“Mikutano ilikuwa ni jambo la kawaida, kila chama kilikuwa na haki ya kufanya mikutano, leo hii hata kufanya mikutano ya ndani difenda za polisi zinazunguka.

“Miaka 13 iliyopita nilikuja Tunduru, tunafanya mikutano ya hadhara na watu wa vyama vyote wanahudhuria na wanasikiliza. Sasa hivi, watu wanaogopa kuja kusikiliza, kwa sababu polisi bila sababu zozote wanazunguka na madifenda,” amesema Zitto.

https://www.youtube.com/watch?v=rp7LlTWnQAU

Kutokana na aliyoieleza Zitto, amesema kuna kila sababu ya kuiondoa Serikali inayotokana na CCM kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba 2020.

“Serikali ya Chama Cha Mapinduzi inapaswa kuondolewa madarakani kwa sababu inaminya haki zenu. Uhuru wenu wa mawazo, Uhuru wenu wa kujieleza, Uhuru wenu wa kuchanganyika, Uhuru wenu wa kukosoa serikali au kusifia serikali umetoweka.

“Leo hii watu hawana Uhuru, ukiongea kitu kuhusu serikali, unajitazama. Sisi 2020 tunazungumzia Uhuru, tumerudi nyuma hatujarudi nyuma?” alipohoji hivyo alijibiwa “tumerudi.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!