May 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Zitto: Katiba ACT-Wazalendo haijavunjwa, ‘tumpigie kura Lissu’

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo

Spread the love

ZITTO Zuberi Kabwe, Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, ameendelea kuwaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi tarehe 28 Oktoba 2020 kumpigia kura Tundu Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chadema. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na MwanaHALISI Online leo Jumatano tarehe 21 Oktoba 2020, Zitto amesema, uamuzi wa kumuunga mkono Lissu ni “maamuzi ya chama kwa mujibu wa vikao.”

Zitto ambaye pia ni mgombea ubunge wa Kigoma Mjini kupitia ACT-Wazalendo amesema katika uamuzi huo wa kumuunga mkono LIssu, katiba ya chama hicho haijavunjwa wala kukiukwa.

Benard Membe, Mgombea Urais kwa tiketi ya ACT-Wazalendo

Katika kusisitiza adhima ya kumuunga mkono Lissu, Zitto amesema, “Watanzania waende kupiga kura kwa wingi na wampigie Tundu Lissu kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”

Zitto na Maalim Seif Sharif Hamad, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo wametangaza licha ya kumsimamisha mgombea urais, Bernard Membe lakini kama chama wameona Lissu ana nguvu za kumtoa mgombea wa CCM, Rais John Pombe Magufuli.

error: Content is protected !!