Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto: Bajeti ya ununuzi ndege, afya ngoma droo
Habari za Siasa

Zitto: Bajeti ya ununuzi ndege, afya ngoma droo

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo
Spread the love

ZITTO Kabwe, Mbunge wa Kigoma Mjini, amekosoa bajeti ya serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/20, kwa kuweka fedha za ununuzi wa ndege kiwango sawa na fedha za kuhudumia afya za Watanzania. Anaripoti Hamis Mguta…(endelea).

Akichambua bajeti ya serikali iliyowasilishwa bungeni na Dk. Philip Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango tarehe 13 Juni 2019, Zitto ambaye ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, mbele ya wanahabari katika Makao Makuu ya chama hicho Kijitonyama, jijiini Dar es Salaam amesema, serikali imelinganisha afya za wananchi kwa kuweka kiwango sawa na ununuzi wa ndege.

“Afya na ndege bajeti yake ni sawa kwa mwaka huu. Madege tunaweka Bilioni 500 na afya za wananchi tunaweka Bil 500,” amesema Zitto.

Amesema kuwa, bajeti ya mwaka huu imewekeza kwenye vitu badala ya kuwekeza kwa wananchi. Akitumia Kitabu namba nne (Book 4), cha Bunge chenye miradi yote ya serikali amesema, kitabu hivyo kinaonesha taswira ya namna serikali ilivyokijita kwenye vitu badala ya watu.

“Kitabu cha Volume 4 (kitabu namba nne) ndicho kilicho na miradi yote ya serikali, bajeti ya mwaka huu ni ya vitu. Asilimia 55.7 ya bajeti yote ya maendeleo imeelekezwa kwenye vitu.

“Kwenye kilimo ambapo ya Watanzania wote wanategemea kilimo, kabajeti kake ndio kale 0.143 yaani Bili 143. Wanasema hii ni serikali ya viwanda lakini fedha walizotenga kwenye wizara hiyo ni 0.051 trilioni yaani bilioni 51.

Amesema, sekta nyingine ya uvuvi ambayo nayo inaajiri watu wengi, imetengewa Sh. 14 bilioni huku maji ikitengewa Sh. 600 Bilioni.

“Sisi tuliotoka kwenye maeneo ya uvuvi Ziwa Tanganyika, Ziwa Viktoria, Ziwa Nyasa na Bahari ya Hindi bajeti yetu ni 0.014 yaan Bil 14…Maji imetengewa Sh. 600 Bilioni huku elimu ikitengewa Sh. 800 Bilioni, katika hizo Bilioni 800, Bilioni 490 hivi ni mikopo ya elimu ya juu,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!