Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto awasusia polisi simu yake
Habari za SiasaTangulizi

Zitto awasusia polisi simu yake

Zitto Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo
Spread the love

ZITTO Kabwe, Mbunge wa Kigoma Mjini amesema kuwa ana mashaka ni kwa nini Jeshi la Polisi linaendelea kushikilia simu yake mpaka sasa na kwamba huenda kuna kitu wanatafuta zaidi ya makosa wanayomtuhumu nayo, anaandika Hamis Mguta.

Simu ya Zitto bado inashikiliwa na polisi na leo kupitia mtandao wake wa Facebook Zitto amewambia wanaomtafuta kwa namba ya simu ya 0767777797 hawawezi kumpata.

Kuchukuliwa kwa simu hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya uchunguzi wa polisi kuhusu tuhuma dhidi yake kwa mujibu wa sheria ya takwimu na sheria ya makosa ya mtandao na polisi walisema watahitaji simu hiyo kwa siku mbili tu.

Ameandika kuwa “Ndugu, jamaa na marafiki, mtakumbuka kuwa mnamo tarehe 7/11/2017 jeshi la polisi walichukua simu yangu kwa ajili ya uchunguzi wao kuhusu tuhuma dhidi yangu kwa mujibu wa sheria ya takwimu na sheria ya makosa ya mtandao.

“Nilikwenda polisi Kamata siku tatu baadaye nikaelezwa kuwa bado wanaendelea na uchunguzi. “Nimerudi leo tarehe 20/11/2017, polisi wanasema bado wanahitaji simu yangu hiyo.

Amewataka watu wanaomtafuta kuktotumia simu ile 0767777797 kwani bado imeshikiliwa na polisi.
Katiba ya nchi yetu kifungu cha 16 (1) na (2) imeweka msingi wa nguvu sana haki ya Faragha kwa raia na kwamba hata sheria ikitaka haipaswi kuingilia mawasiliano binafsi ya Raia.

“Nina mashaka kuwa jeshi la polisi linakaa na siimu yangu muda wote huu kwa sababu za zaidi ya uchunguzi wao wa makosa wanayonituhumu nayo.

“Nimeamua kuwaachia simu mpaka hapo watakapotosheka lakini wajiandae na kesi ya kikatiba ambayo pia italinda haki za wananchi wengi wanaothirika na matumizi mabaya ya sheria ya mtandao (Cybercrime act).”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

Regina Mkonde: CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!