Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT-Wazalendo ‘yawapiga stop’ wabunge wake kwenda bungeni
Habari za Siasa

ACT-Wazalendo ‘yawapiga stop’ wabunge wake kwenda bungeni

Spread the love

KIONGOZI wa chama cha upinzani nchini Tanzania, ACT-Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe amesema, wananchi wasitegemee kuwaona wabunge wa chama hicho wakienda bungeni. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea)

Zitto amesema, chama hicho kwa sasa hakiwazi suala la ruzuku au wabunge wa viti maalum na kimejikita kufuatilia wananchi na viongozi wao waliojeruhiwa na kushikiliwa kutokana na vurugu za Uchaguzi Mluu wa tarehe 28 Oktoba 2020.

Katika uchaguzi huo, kati ya majimbo 264, ACT-Wazalendo imejipatia majimbo matatu ya Pemba-Zanzibar.

Zitto amesema hayo leo Jumapili tarehe 8 Novemba 202 wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisi za chama hicho, Magomeni jijini Dar es Salaam.

Amesema, zaidi ya wanachama 169 nchi nzima “wamekamatwa katika siku ambazo zimepita na bado wanaendelea kukamatwa, mwenyekiti wetu (Maalim Seif Sharif Hamad) alikamatwa na mimi mwenyewe nilikamatwa na tunaendelea kuripoti polisi.”

Kiongozi huyo amesema, Nasaor Mazrui, naibu katibu mkuu wa chama hicho (Zanzibar) pamoja na wenzake walikamatwa huku Mazrui akipigwa na kumfanya kupoteza fahamu na “polisi walikiri wanaye na mimi mwenyewe juzi Ijumaa nimekwenda ofisi ya DCI nikazungumza na naibu wake akatuthibitishia wanaye Mazrui pamoja na wengine nane.”

Zitto aliyekuwa mgombea ubunge Kigoma Mjini amesema “Ismail Jusa jana amefanyiwa upasuaji wa bega nchini Nairobi-Kenya uliochukua saa saba pamoja na mguu wake uliokuwa umevunjika baada ya kupigwa alipokamatwa. Upasuaji ulimalizika salama.”

Kutokana na hyo, Zitto amesema “kwetu sisi hapakuwa na uchaguzi na kuna taratibu zinaendelea kufanywa ndani ya chama kwa wale waliotangazwa kushindwa, lakini msitegemee kuona wabunge na madiwani waliotokana na ACT-Wazalendo bungeni.”

“Hakuna jambo ambalo ni muhimu zaidi ya uhai wa watu, kiongozi mwenzangu (Mazrui) sijui anaendeleaje, sasahivi siwazi ruzuku, viti maalum wala chochote, nachowaza ni damu ya wanachama wangu na uhai wa viongozi wangu,” amesema.

9 Comments

  • Mbona wao hao viongozi wa upinzani waliposhinda miaka iliyopita na kudai kuwa upigaji kura haukuwa wa haki lakini walihudhuria Bungeni mara mara na walipopigwa hawakuacha kuhudhuria bunge, lakini leo wao wameshindwa wanaagiza wanachama wao waliopigiwa kura za ushindi na watanzania wengi na wa vyama mbalimbali wasihudhurie bunge, kulikoni!

  • Mi naona wasiende maana yatakua mazoea Kama kwel Kuna sehemu yakulinda haki za binadamu jamani zitusaidie kutoa kiongozi mmoja wa chadema Kama mbunge sio kwamba Ni haki uwo nikama mtego tu wasemehe Kuna upinzani bungeni naombeni viongozi tutaftie haki zetu sisi tuliopiga kura tunaumia Sana kunyanganywa haki yetu tunalazimishwa viongozi tusiowataka kuanzia serikali za mitaa Tanzania tunaenda wap jaman

  • Chadema wakumbuke Siraha alikuta chama kina wabuge 2, Mbinu alizotumia mpaka mkapata wabuge zaidi ya 30. kwa muda wa miaka 10. tumia hizo hizo.
    Fikilia nje ya box sio kutokwenda bungeni.
    Mwsho wa siku hutakuta chama hakipo tena
    KAMA MNATAKA CHAMA KIWEPO NENDENI BUGENI

  • Tusifanye maamuzi kwa jazba kwa sababu hasira ni hasara. Miaka yote chadema na ACT hawajawahi kukubali matokeo ya uchaguzi lakini wabunge walioshina wakiwemo Mbowe na Zitto walikwenda bungeni. Vipi Leo kwa vile tu wao hawajuchaguliwa wanawatoa kafara hao walioshinda safari hii,? Kwa mini wao walikwenda? Wao in nani na hao ni nani. Hii itawaketea mgawanyiko mkubwa ktk. Vyama vyao

  • We nae unashindwa kuelewa Zama hizo kikwete alikuwa mtu wa diplomasia hakuwa Kama huyu bwana unaongea eti njia za Dr slaa hakuna njia yoyote uwanja wa democracy ulikuwa Kama uko wazi asilimia 98

  • Nyinyi wengine hamna akili hivi kwe ww kwa Tanzania au Zanzibar zaid wapinzan km maalim seif Sharif Hamad akose hata viti ishirini 20 hiyo ni ajabu kubwa Tanzania ninchi ilio na upinzan kuliko nchi nyingi dunia zaid wakati tulionao na viongoz wa kiserekali wanaotumia nguvu ya dola zaid kuliko Sheria au katiba wanalazimisha kuka madarakan bila haki na ridhaa ya wananchi hiyo sio sawaaaaa jamaniiiiiiiii

  • Ni lazima uchaguzi urudiwe jamani sio haki ara kidogo kwa walivofanyiwa vyama vya upinzani mwaka huu ni dhulma kubwa sana kupita maelezo.

  • Ukweli ni huu. CCM licha yakuiba nakupiga kura kabla ya siku 28.11.20 matokeo yulionayo baada yakuhakiki ni hayo
    Chadema 7,534,301=64%
    Ccm 6,423,694=34%
    ACT 2,69,002=1.5%
    Chama 94,691

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!