Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto amharibia JPM Kigoma
Habari za Siasa

Zitto amharibia JPM Kigoma

Zitto Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo akizungumza na wananchi wa Kigoma
Spread the love

ZITTO Kabwe, Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, amemchomea utambi Rais John Magufuli kwamba, amewatupa watu wa Kigoma. Anaripoti Faki Sosi, Kigoma … (endelea).

Amesema, Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imehamisha fedha za mradi wa umeme wa Malagarasi na kuzipeleka katika mradi wa umeme Stigler Gorge, Rufiji mkoani Pwani.

Amesisitiza, kwamba endapo wananchi wa Kigoma watathubutu kuichagua CCM, watakuwa wamechagua kuendelea kutengwa.

Zitto ametoa kauli hiyo mkoani Kigoma akiwa kwenye ziara yake ya Mikoa ya Magharibi, aliyoianza mwanzoni mwa wiki hii.

“Nyinyi mnafahamu, tulikuwa na mradi mkubwa wa kuzalisha umeme wa maji hapa Kigoma. Mradi wa umeme wa Malagarasi wa Megawati 43.

“Ukisoma Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi mwaka 2015, wameahidi ifikapo 2020 mradi wa umeme wa maji wa Malagarasi utakuwa umekamilika,” amesema Zitto.

Amesema, akiwa bungeni alimuuliza Dk. Medard Kalemani, Waziri wa Nishati kuhusu mradi huo, majibu yake yalikuwa fedha hizo zimeelekezwa katika mradi wa Stigler Gorge.

“Mwaka 2020, mimi nimeuliza ndani ya Bunge, nimemuuliza Waziri wa Nishati, Mradi wa Umeme wa Malagarasi ambao tulikuwa tumekwishapewa fedha na Benki ya Maendeleo ya Afrika umefikia hatua gani?

“Waziri akasema, sasa hivi serikali inafanya mradi mmoja tu wa Stigler Gorge, kwa hiyo fedha za mradi wa umeme wa Malagarasi Kigoma wamepeleka knweye Stigler Gorge, sisi tumeachwa,” amesema Zitto.

Rais John Magufuli

Akisisitiza umuhimu wa mradi huo, Zitto amesema ulitarajiwa kuzalisha Megawati 43 ana kwamba, kw amatumizi ya Kigoma ambayo hayaziti Megawati 20, Kigoma ingeweza kuuza umeme Burundi.

“Sisi umeme wetu wa Malagarasi ni Megawati 43, matumizi ya Kigoma hayazidi Megawati 20, tungeweza kuwauzia hata Burundi. Watu wa Kigoma mkichagua CCM, maana yake mmekubali kuendelea kutengwa,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!