Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto aitwanga barua Takukuru
Habari za Siasa

Zitto aitwanga barua Takukuru

Spread the love

ZITTO Kabwe amemuandikia barua ya malalamiko Diwani Athuman, Kamishna wa Polisi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kutokana na usumbufu alioupata kutokana na maagizo ya taasisi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Zitto ambaye ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, amechukua hatua hiyo siku mbili baada ya kuzuiwa na Mamlaka ya Uhamiaji Zanzibar, kwenda Mombasa nchini Kenya kwa safari zake binafsi, kwa kile kilichoelezwa kwamba ni maagizo kutoka Takukuru.

“Baada ya kuuliza, nikafahamishwa na Naibu Kamishna wa Polisi Zanzibar kwamba, nimetuhumiwa na Takukuru kwa mujibu wa sheria ya huduma ya habari ya mwaka 2016, hivyo polisi kwa niaba ya Takukuru walichukua simu yangu ya mkononi na kompyuta yangu,” inaeleza sehemu ya barua ya Zitto.

Katika sehemu ya barua hiyo, Zitto ameonesha kushangzwa na kanusho lililotolewa na taasisi hiyo kupitia kwa Naibu Mkurugenzi wa Takukuru, aliyenukuliwa na vyombo vya habari akisema kwamba, taasisi hiyo haijatoa maagizo yoyote dhidi ya zuio la safari ya mwanasiasa huyo.

“Taarifa hiyo imenishangaza sana kwani ninaamini kuwa, Polisi na Uhamiaji Zainzibar hawawezi kamwe kuchukua hatua walizochukua na kuwazushia Takukuru, ninaamini kuwa ofisi yako inachezea wananchi kwa kukanusha jambo ambalo hakika mmelifanya,” inaeleza sehemu ya barua ya Zitto kwa Kamishna Athumani.

Katika barua yake hiyo aliyoandika leo tarehe 13 Juni 2019, Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini aliiomba Takukuru imfikishe mahakamani kwa ajili ya kuuomba mhimili huo ruhusa ya kumzuia kusafiri nje ya nchi kwa mujibu wa sheria, kama anatuhumiwa na taasisi hiyo.

Pia, ameiomba Takukuru iondoe zuio la yeye kusafiri nje ya nchi mara moja katika mfumo wa uhamiaji, ili aweze kufanya shughuli zake kama raia na kiongozi bila vikwazo.

Hali kadhalika Zitto ameiomba Takukuru kuhakikisha kwamba, simu na kompyuta yake iliyochukuliwa, arejeshewe pamoja na kuombwa radhi kwa usumbufu alioupata

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!