Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto ahoji matokeo uchunguzi maabara ya Corona 
Habari za Siasa

Zitto ahoji matokeo uchunguzi maabara ya Corona 

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo
Spread the love

ZITTO Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, amehoji matokeo ya kamati iliyoundwa kuchunguza sakata la vipimo vya ugonjwa wa homa kali ya mapafu, inayosababishwa na virusi vya corona (Covid-19). Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Kamati hiyo ya wataalamu nane wabobezi wakiongozwa na Prof. Eligius Lyamuya kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, iliundwa tarehe 4 Mei 2020 na Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, na kutakiwa kuwasilisha taarifa yake kabla ya tarehe 13 Mei, 2020.

Waziri Ummy aliunda kamati hiyo sambamba na kuwasimamisha kazi, Dk. Nyambura Moremi, aliyekuwa Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii na Jacob Lusekelo, Meneja Udhibiti wa Ubora, ili kupisha uchunguzi.

Waziri Ummy alichukua hatua hiyo kwa ajili ya kutekeleza agizo la Rais John Magufuli, la kuifanyia uchunguzi  maabara hiyo kuhusu mfumo wake wa ukusanyaji na upimaji wa sampuli za Covid-19.

Rais Magufuli alitoa agizo hilo tarehe 3 Mei 2020, akiwa Chato mkoani Geita, baada ya vyombo vya usalama kubaini dosari za vipimo hivyo, ambapo vilionyesha sampuli za wanyama na matunda kuwa na maambukizi ya Covid-19.

Leo tarehe 21 Mei 2020, ikiwa siku nane zimepita bila ya taarifa ya matokeo ya uchunguzi wa kamati hiyo kuwekwa wazi, Zitto amehoji mustakabali wa uchunguzi huo.

Dk. Nyambura Moremi, aliyekuwa Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa ya Afya

Akizungumza na Watanzania kwa njia ya mtandao, Zitto amedai, uchunguzi huo umepelekea Tanzania kutotangaza taarifa za wagonjwa wa Covid-19.

“Licha ya kuwa tangazo la ubovu wa vifaa ilikuwa wazi, lakini mpaka leo kamati ile haijaweka wazi taarifa ya uchunguzi wake. Kutokana na hatua hiyo Serikali (ya Jamhuri ya Muungano) haijatangaza taarifa za wagonjwa wa Corona tangu tarehe 29 Aprili, 2020,” amesema Zitto.

Tarehe 8  Mei 2020, Waziri Ummy alisema Tanzania imesimama kutoa takwimu za mwenendo wa Covid-19 nchini, kutokana na maabara iliyokuwa inapima sampuli za ugonjwa huo kufanyiwa marekebisho.

Zitto amesema, kusimama kwa utoaji wa takwimu hizo, kumepelekea baadhi ya wananchi kupuuza matokeo ya vipimo vya ugonjwa huo.

“Mbali na kwamba habari hiyo ya vipimo vya Corona kuwa na kasoro haikuwa habari mpya, kwani kote duniani kasoro zimebainika; habari hiyo iliyopewa kipaumbele na Mheshimiwa Rais imeidogosha nafasi ya sayansi katika jamii yetu,” amesema Zitto na kuongeza:

“Na matokeo yake, wananchi sasa wanaamini matokeo yote ya vipimo vya Corona si sahihi, isipokuwa majibu yakiwa ni “Negative”, Tunadhani hii ni hatari sana katika ujenzi wa taifa la kisasa, ni kurudi katika enzi za ujima na dunia ilipokuwa na maarifa machache.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

error: Content is protected !!