Zitto Kabwe, Mwenyekiti wa chama cha ACT-Wazalendo

Zitto aanzisha mashambulizi CCM, serikali

ZITTO Kabwe, Mbunge wa Kigoma Mjini ameivaa serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwamba ni katili. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kwenye ukurasa wake wa Twitter Zitto ameeleza kushangazwa na ukimya wa CCM wakati wakulima wa korosho wakiteketea.

Zitto ameandika; “Serikali katili inadhulumu jasho la Wananchi masikini. Wakulima wanarejeshewa Korosho zao sasa.

“CCM hawawezi hata kupaza sauti kukemea ukatili unaofanywa na Serikali yao. Dhulma kwa mtu mnyonge ni mbaya sana.”

Serikali hivi karibuni imetangaza kufungua milango kwa wafanyabiashara wa korosho kwenda kununua zao hilo.

Katika msimu huu zao hilo limeingia mdudu baada ya kuwepo mvutano wa bei ya ununuzi ambapo serikali iliingilia katika na kununua zao hilo.

Hata hivyo, malalamiko kwa serikali kushindwa kukidhi ununuzi huo yamekuwa yakisikika.

Miongoni mwa wabunge wanaoishutumu serikali kufanya uzembe katika ununuzi wa zao hilo hivyo kutaabisha wakulima ni Nape Nnauye, Mbunge wa Mtama, Suleiman Bungara (Kilwa Kusini) na Hawa Ghasia (Mtwara Vijijini).

ZITTO Kabwe, Mbunge wa Kigoma Mjini ameivaa serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwamba ni katili. Anaripoti Mwandishi Wetu ... (endelea). Kwenye ukurasa wake wa Twitter Zitto ameeleza kushangazwa na ukimya wa CCM wakati wakulima wa korosho wakiteketea. Zitto ameandika; "Serikali katili inadhulumu jasho la Wananchi masikini. Wakulima wanarejeshewa Korosho zao sasa. "CCM hawawezi hata kupaza sauti kukemea ukatili unaofanywa na Serikali yao. Dhulma kwa mtu mnyonge ni mbaya sana." Serikali hivi karibuni imetangaza kufungua milango kwa wafanyabiashara wa korosho kwenda kununua zao hilo. Katika msimu huu zao hilo limeingia mdudu baada ya kuwepo mvutano wa bei ya ununuzi ambapo…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

error: Content is protected !!
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On YoutubeVisit Us On Instagram