Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto aachiwa kwa dhamana, akamatwa tena, sasa takwimu
Habari za SiasaTangulizi

Zitto aachiwa kwa dhamana, akamatwa tena, sasa takwimu

Zitto Kabwe, Mwenyekiti wa chama cha ACT-Wazalendo
Spread the love

KIONGOZI wa Chama Cha ACT-Wazalendo ameachiwa kwa dhamana alipokuwa anahojiwa katika kituo cha Polisi cha Chang’ombe kwa madai ya kutoa maneno ya uchochezi, kabla ya kukamatwa tena sasa kwa makosa ya kutoa takwimu, anaandika Faki Sosi.

Zitto ambaye alikamatwa mapema asubuhi na kupelekwa katika kituo cha Chang’ombe kwa mahojiano, lakini alipoachiwa kwa dhamana alikamatwa tena na polisi na kupelekwa katika kituo cha polisi Kamata, Kariakoo kwa mahojiano ya takwimu alizozitoa wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa Katibu wa Itakadi na Uenezi wa cha hicho, Ado Shaibu amesema kuwa chama Zitto amehojiwa na Polisi kwa kutuhumiwa kutoa maneno ya uchochezi kwenye kampeni za udiwani Kata ya Kijichi, Temeke.

Shaibu amesema kiongozi wao aliachiwa majira ya saa sita kwenye kituo hicho na kukamatwa tena na kupelekwa kwenye kikosi maalumu cha Kamata.

Mawakili waliomsindikiza Zitto kwenye mahojiano hayo ni pamoja na Steven Mwakibolwa na Venas Msebo ambao wamefuatana naye tena katika kituo cha polisi Kamata.

Kwenye kituo cha Polisi cha Chang’ombe Zitto amedhaminiwa na wadhamini wawili kwa sharti la kurudi tena kituoni hapo Jumatatu.

Aidha, Polisi wanaendelea na mahojiano na Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo ndugu Zitto Kabwe baada ya kumuachia Kituo cha Chang’ombe kwa dhamana na kumtaka arudi siku ya Jumatatu, na kisha kumkamata tena na kumpeleka  kwa mahojiano katika kituo cha Polisi cha Kamata.
Mahojiano ya sasa yanahusisha tuhuma mbili:
Tuhuma ya kwanza inayomkabili Zitto ni kuchapisha takwimu kinyume na Kifungu cha 37(5) ya Sheria ya Takwimu 2015, Polisi wakitafsiri kuwa kusoma kwake taarifa ya Kamati Kuu ya ACT Wazalendo iliyoelezea takwimu za Serikali juu ya hali ya uchumi wa nchi kusinyaa, kuwa ni kuchapisha Takwimu.
Na tuhuma ya pili ni kusambaza taarifa hiyo ya Uchambuzi ya Takwimu ya Kamati Kuu ya ACT Wazalendo kwenye mitandao ya Kijamii kinyume na Kifungu cha 16 cha Sheria ya Mitandao ya Kijamii (Cyber Crime Act).
Hivyo basi, mpaka sasa jumla ya tuhuma zinazomkabili ni nne, kwa kuunganisha zile mbili za awali za Uchochezi kwa kuwakataza wananchi wasiichague CCM kwa sababu mpaka leo Serikali ya CCM imeshindwa kuwakamata waliompiga risasi Lissu pamoja na kushindwa kujua chanzo cha maiti mbalimbali zinazookotwa katika ufukwe wa Coco Beach.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

error: Content is protected !!