ZFF yamlilia ‘Mr White’

Spread the love

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) kupitia rais wake Seif Kombo Pandu imetoa pole na kutuma salamu za rambi rambi kufuatia kifo cha Salim Abdullah Turky ‘Mr White’ ambaye alikuwa mbunge aliyemaliza muda wake katika jimbo la Mpendae, Unguja kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Mwandishi Wetu, Unguja … (endelea).

Mr White alikutwa na umauti usiku wa kuamkia leo, Terehe 15 Septemba, mjini Unguja.

Katika salamu zake za rambi rambi Rais wa ZFF, Seif Pandu ameeleza kuwa marehemu Turky atakumbukwa katika jitihada za kusaidia mchezo wa mpira wa miguu na baadhi ya timu pale msaada wake utakapohitajika. 

Salim Turky, aliyezaliwa 11 Februari 1963, mjini Unguja, anatarajiwa kuzikwa jioni ya leo, kijijini kwake, Fumba, takribani umbali wa kilomita 65 kutoka jimboni kwake, Mpendae, wilaya ya Mjini Magharibi.

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) kupitia rais wake Seif Kombo Pandu imetoa pole na kutuma salamu za rambi rambi kufuatia kifo cha Salim Abdullah Turky ‘Mr White’ ambaye alikuwa mbunge aliyemaliza muda wake katika jimbo la Mpendae, Unguja kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Mwandishi Wetu, Unguja ... (endelea). Mr White alikutwa na umauti usiku wa kuamkia leo, Terehe 15 Septemba, mjini Unguja. Katika salamu zake za rambi rambi Rais wa ZFF, Seif Pandu ameeleza kuwa marehemu Turky atakumbukwa katika jitihada za kusaidia mchezo wa mpira wa miguu na baadhi ya timu pale msaada wake utakapohitajika.  Salim Turky,…

Review Overview

User Rating: 1 ( 1 votes)

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!