Thursday , 28 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa ZANU PF yamshinikiza Mugabe ajiuzulu
KimataifaTangulizi

ZANU PF yamshinikiza Mugabe ajiuzulu

Robert Mugabe, Rais wa Zimbabwe
Spread the love

CHAMA tawala Zimbabwe ZANU PF kimemtaka Rais Robert Mugabe ajiuzulu, kauli hiyo imetolewa na viongozi wa matawi ya chama hicho katika majimbo yote 10 yaliyokutana jana na yamemtaka Mugabe na mke wake Grace wajiuzulu.

Viongozi wa chama hicho wamesema watamshinikiza kiongozi huyo ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1980 kuondolewa kutoka uongozi wa chama hicho ifikapo hapo kesho Jumapili na baada ya hilo, bunge litapiga kura ya kutokuwa na imani naye.

Chama cha ZANU PF kitafanya mkutano maalamu wa kamati kuu siku ya Jumapili kujadili yanayojiri kisiasa nchini humo.

Mugabe alionekana kwa mara ya kwanza hadharani, katika mahafali ya chuo kikuu mjini Harare siku ya jana tangu jeshi lilipomuweka chini ya kifungo cha nyumbani wiki hii. Mkewe Grace hajaonekana hadharani tangu jeshi lilipochukua madaraka.

Jeshi la Zimbabwe linapata ugumu wa kuonyesha heshima kwa kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 93 kwa kumuita rais na kamanda mkuu wa jeshi.

Taarifa kutoka kwa jeshi hilo imesema kuwa viongozi wake wanashauriana na Kamanda Mkuu wa jeshi Rais Robert Mugabe kuhusu njia bora ya kusonga mbele na litalifahamisha taifa baadaye kuhusu matokeo hayo haraka iwezekanavyo.

Kituo cha televisheni cha serikali ZBC kimeripoti kuhusu kuendelea kwa shinikizo kutoka kwa wanachama wa ZANU PF kwa Mugabe kujiuzulu. ZBC imekuwa ikitumika na serikali ya Mugabe kwa miongo kadhaa kueneza propaganda.

ZANU PF pia imeitisha maandamano leo katika mji mkuu, Harare kuliunga mkono jeshi kwa kuchukua madaraka na kumshinikiza Mugabe ajiuzulu.

Wananchi wa Zimbabwe wakiandama katika jiji la Harare wakishinikiza Rais Robert Mugabe ajihudhuru

Pia chama hicho kinataka makamu wa Rais aliyefutwa kazi Emmerson Mnangagwa arejeshwe katika wadhifa huo kwa sababu alifutwa kazi bila ya ridhaa ya kamati kuu ya chama hicho.

Wazimbabwe wengi wanahisi mipango ya jeshi ni kumkabidhi Mnangagwa madaraka. Huenda viongozi wa kijeshi wanasubiri Mnangagwa ambaye anajulikana kwa jina maarufu kama mamba arejeshwe katika wadhifa wa makamu wa rais kabla ya kumshinikiza Mugabe kuondoka madarakani kwa njia ya amani.

Mugabe anaheshimika sana kama kiongozi aliyepigania uhuru lakini pia wengi wanamuona kama Rais aliyeivuruga nchi yake kwa kusalia madarakani kwa muda mrefu.

Uchumi wa nchi hiyo umeporomoka vibaya, visa vya ufisadi, usimamizi mbaya, azma ya mke wake Grace kutaka kurithi madaraka na umri wake kuwa mkubwa ni mambo yanayowafanya Wazimbabwe kuhisi hana uwezo tena wa kuliongoza taifa hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

Habari za SiasaTangulizi

CAG aibua madudu halmashauri 10, TANESCO na MSD

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!