Zamu ya Dola kumdhibiti Maalim

Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) visiwani Zanzibar kimeshindwa kumdhibiti Maalim Seif Sharif Hamad na sasa dola kutumika, anaandika Faki Sosi.

Wabunge wa CCM kupitia Baraza la Wawakilishi (BLW) visiwani humo jana walipitisha hoja kuwa Maalim Seif adhibitiwe na vyombo vya dola kwa madai ya kusababisha uchochezi kwa wananchi.

Hoja hiyo binafsi iliwasilishwa na Mtumwa Pea Yusuf, Mbunge wa Jimbo la Mpendae, Unguja akiitaka Serikali ya CCM na vyombo vyake vya dola ‘kumshughulikia’ Maalim Seif ambaye alikuwa mgombea urais visiwani humo kupitia Chama cha Wananchi (CUF) katika uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba mwaka jana.

Katika baraza hilo la upande mmoja (CCM), wajumbe wote walipitisha hoja hiyo kwa shangwe wakilenga kupunguza kasi ya Maalim Seif ambayo inamwathiri Dk. Ali Mohammed Shein katika serikali yake.

Tangu kumalizikwa kwa uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka jana na matokeo yake kuvurugwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kwa maslahi ya Dk. Shein ambaye ni mgombea wa CCM, Maalim Seif amekuwa mwiba visiwani humo.

Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) visiwani Zanzibar kimeshindwa kumdhibiti Maalim Seif Sharif Hamad na sasa dola kutumika, anaandika Faki Sosi. Wabunge wa CCM kupitia Baraza la Wawakilishi (BLW) visiwani humo jana walipitisha hoja kuwa Maalim Seif adhibitiwe na vyombo vya dola kwa madai ya kusababisha uchochezi kwa wananchi. Hoja hiyo binafsi iliwasilishwa na Mtumwa Pea Yusuf, Mbunge wa Jimbo la Mpendae, Unguja akiitaka Serikali ya CCM na vyombo vyake vya dola ‘kumshughulikia’ Maalim Seif ambaye alikuwa mgombea urais visiwani humo kupitia Chama cha Wananchi (CUF) katika uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba mwaka jana. Katika baraza hilo la upande mmoja (CCM),…

Review Overview

User Rating: Be the first one !
0

About Faki Sosi

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube