Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Michezo Yanga yatangaza kocha mpya
Michezo

Yanga yatangaza kocha mpya

Zlatko Krmpotic
Spread the love

MABINGWA wa kihistoria nchini Tanzania, Yanga, imemtangaza Zlatko Krmpotic kuwa Kocha Mkuu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Kocha huyo anakuja kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Luc Eymael raia wa Ubelgiji aliyetimuliwa tarehe 27 Julai 2020 kutokana na kutuhumiwa kutoa lugha zisizo za kiungwana.

Yanga imejikuta ikitua kwa raia huyo wa Serbia baada ya kushindwa kuelewana na Cedrick Kaze raia wa Burundi.

Kaze alikuwa awasili Tanzania leo Ijumaa tarehe 28 Agosti 2020 kuanza kibarua kipya ndani ya timu hiyo ya Jangwani, Dar es Salaam lakini akatoa udhuru na kutaka apewe wiki tatu zaidi ili kumaliza matatizo ya kifamilia yaliyokuwa yakimsibu.

Lucy Eymael

Hata hivyo, Yanga haikukubaliana na ombi hilo na kuamua kutua kwa Krmpotic ambaye amehudumu kama kocha katika nchi 12 tofauti ikiwemo DR Congo katika timu ya TP Mazembe akiwa kocha msaidizi na kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Timu zingine alizozifundisha ni; APR ya Rwanda na Zesco ya Zambia  na timu ya mwisho mwisho kuifundisha ni Polokwane City FC ya Afrika Kusini.

Krmpotic atakuwa akisaidiwa na kocha msaidizi, Juma Mwambusi ambaye ndiye anayekinoa kwa sasa.

Zlatko Krmpotic

Yanga inaendelea na sherehe za “Wiki ya Mwananchi’ ambayo kilele chake kitahitimishwa Jumapili tarehe 30 Agosti 2020 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Siku hiyo, kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali akiwemo, Rajab Abdul Kahali maarufu Harmonize au ‘Konde Boy.’

Pia, kutakuwa na utambulisho wa wachezaji watakaotumika msimu wa 2020/21 na mwisho siku, itahitimishwa kwa mchezo wa kirafiki utakaochezwa dhidi ya Aigle Noir ya Burundi huku mgeni rasmi akiwa Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Tusua mkwanja na mechi za Ijumaa leo

Spread the love  LEO hii mechi zinaendelea kote na wewe kama unataka...

Michezo

Piga pesa na mechi za EUROPA leo hii

Spread the love Hatimaye Alhamisi ya EUROPA imefika ambapo leo hii mechi...

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

error: Content is protected !!