Wednesday , 24 April 2024
Home Kitengo Michezo Yanga yamshushia rungu Lamine Moro
Michezo

Yanga yamshushia rungu Lamine Moro

Spread the love

KLABU ya Yanga imewaomba radhi kiungo wa JKT Tanzania, Mwinyi Kazimoto na tiju yake, huku ikimwadhibu beki wake, Lamine Moro raia wa Ghana, kwa kitendo cha utovu wa nidhamu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Lamine ameadhibiwa kwa kukatwa Tsh. 1,000,000 kwenye mshahara wake mara baada ya kuonesha kitendo kisicho cha uungwana kwa kumpiga teke Kazimoto. 

Kitendo hicho kilichomfanya beki huyo kutolewa nje na mwamuzi Lodivic Charles kutoka Mwanza, kwa kumuoneshea kadi nyekundu katika dakika 89 ya mchezo.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo iliyotoka muda mfupi mara baada ya mchezo huo kukamalika imeeleza kuwa, licha ya mchezaji huyo kuomba radhi lakini uongozi umeamua kumchukulia hatua kwa mujibu wa kanuni na taratibu za klabu.

Lakini pia Yanga imeomba radhi kwa wapenzi wa mpira wa miguu nchini sambamba na kiungo wa klabu ya Jkt Mwinyi Kazimoto.

Lamine Moro ataoukosa mchezo ujao dhidi ya Azam FC utakaofanyika siku ya Kumapili, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

Michezo

Ujanja ni kubeti na Meridianbet

Spread the love  JUMAPILI ya leo imekaa kihela hela sana ndani ya...

Michezo

Anza Jumamosi yako na mkwanja wa Meridianbet

Spread the loveJumamosi ya leo ODDS zimekaa kijanja sana ndani ya Meridianbet...

error: Content is protected !!