Mashabiki wa Yanga

Yanga yalaani kufanyiwa vurugu mashabiki wa Simba

Spread the love

KLABU ya soka ya Yanga imelaani vikali kitendo cha mashabiki wao kuwafanyia vurugu mashabiki wa klabu ya Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa uliochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Katika taarifa yao uongozi wa klabu ya Yanga unalaani tabia hiyo kutoka kwa mashabiki wao inayojengeka na kuvitaka vyombo vya ulinzi kuchunguza na kuchukua hatua kwa wale wote watakaobainika.

Tukio la aina hiyo litakuwa kwa mara ya pili kwa msimu kwa mashabiki wa klabu ya Yanga kuwafanyia fujo mashabiki wa Simba kwenye michezo mbalimbali.

Ikumbukwe katika kilele cha siku ya tamasha la wiki ya mwananchi lililofanyika 30 Agosti, 2020. kulitokea tukio la aina hii ambapo baadhi ya mashabiki wa Yanga walionekana kumchania jezi shabiki wa samba aliyefika kiwanjani kuangalia mchezo wa kirafiki kati ya Yanga na Aigle noir ya nchini Burundi.

Uongozi wa klabu hiyo pia umeendelea kusisitiza kuwa mchezo wa mpira wa miguu ni mchezo wa furaha na sio uadui kwani upinzani wao na Simba unataokana na utani wao wa jadi na sio uhasama.

Katika mchezo huo Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Mtibwa na kujipatia pointi tatu na kufikisha alama 10 sawa na Simba wakitofautiana magoli ya kufungwa na kushinda.

KLABU ya soka ya Yanga imelaani vikali kitendo cha mashabiki wao kuwafanyia vurugu mashabiki wa klabu ya Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa uliochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam ... (endelea). Katika taarifa yao uongozi wa klabu ya Yanga unalaani tabia hiyo kutoka kwa mashabiki wao inayojengeka na kuvitaka vyombo vya ulinzi kuchunguza na kuchukua hatua kwa wale wote watakaobainika. Tukio la aina hiyo litakuwa kwa mara ya pili kwa msimu kwa mashabiki wa klabu ya Yanga kuwafanyia fujo mashabiki wa Simba kwenye michezo mbalimbali. Ikumbukwe katika kilele…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!