MABINGWA wa kihistoria wa soka nchini Tanzania, Yanga ya jijini Dar es Salaam, wamezindua jezi mpya ambazo zitatumika katika msimu wa 2020/21. Anaripoti Kelvin Mwapungu, Dar es Salaam … (endelea).
Uzinduzi huo umefanyikia makao makuu ya timu hiyo, Jangwani leo Ijumaa tarehe 11 Septemba, 2020 na kuhudhuriwa viongozi mbalimbali wa Yanga akiwemo Makamu Mwenyekiti wake, Fredrick Mwakalebela na Mshauri wa timu hiyo, Senzo Mazingisa.
Yanga imekuwa klabu ya kwanza Tanzania kuwa na duka lake la vifaa vya michezo katika makao ya timu ambapo, Senzo amewaomba mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kununua ili kuongeza mapato ya timu na kuifanya kuendelea kuwa bora zaidi ndani na nje ya Tanzania.
Senzo amesema huo ni mwelekeo mzuri wa timu kuwa na duka lake la vifaa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa GSM, Hersi Said amesema, kila mwaka watakuwa wanatengeneza jezi nzuri “hatutengenezi jezi tu bora tumetengeneza” na zitakuwa zinaendena na tamaduni za Kiafrika na ki-Yanga.
Leave a comment