Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Michezo Yanga wamkatia rufaa Morrison Fifa
Michezo

Yanga wamkatia rufaa Morrison Fifa

Frederick Mwakalebela, Makamu Mwenyekiti wa Yanga
Spread the love

MUDA mchache baada ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kutoa maamuzi ya kesi ya kimkataba kati ya klabu ya Yanga na Bernard Morrison, klabu hiyo haijardhishwa na uamuzi na kuamua kukata rufaa. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea). 

Yanga imeanua kukataa rufaa kwenye mahakama ya kimataifa ya usuluhisho wa michezo (CAS) iliyokuwa chini ya Shirkisho la Soka Duniani (FIFA). 

Baada ya kesi hiyo kusikilizwa kwa siku tatu, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Elias Mwanjala amesema kamati yake imebaini kuwa mkataba ulioletwa na Yanga na kudaiwa ulisainiwa na mchezaji huyo, kuonekana kuwa na mapungufu na kufanya mkataba huo kutoonekana kuwa halali na mchezaji huyo kuachiwa huru.

Mara baada ya maauzi hayo,  klabu ya Yanga kupitia mitandao yao ya kijamii ilitoa taarifa ya kukataa rufaa juu ya shauli hilo kutokana na kutoridhishwa na uamuzi huo na kuamua kwenda ngazi za juu ili kutafuta haki.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa uongozi wa klabu hiyo unakusudia kukata rufaa CAS mara baada ya kupata nakala ya hukumu kutoka kamati husika na kutaka wanachama wa klabu hiyo kutulia katika kipindi hiki.

Yanga ilimleta nchini Morrison 17 Januari, 2020 kwenye dirisha dogo la usajili kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo kwa mkataba wa miezi sita kabla ya kuingia katika mgogoro.

Licha ya Yanga kutaka kukata rufaa lakini mpaka sasa Morrison anahesabika kama mchezaji wa klabu ya Simba baada ya kuingia nao mkataba wa miaka miwili.

Aidha mchezaji huyo atapelekwa kwenye kamati ya nidhamu kutoa maelezo ya kwanini asaini mkataba na klabu ya Simba huku bado kukiwa na kesi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Makala & UchambuziMichezo

TFF kuamua hatima ya Amrouche

Spread the loveHATIMA ya Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche kuendelea...

Habari za SiasaMichezo

Matinyi: Dk. Ndumbaro alifanya utani ukaguzi mechi za Yanga, Simba

Spread the loveMsemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema kauli iliyotolewa na...

Michezo

Gethsemane Group Kinondoni (GGK) waachia video ya Bwana Wastahili

Spread the loveWAIMBAJI maarufu nchini kutoka Gethsemane Group Kinondoni (GGK)SDA wameachia video...

BiasharaMichezo

Gamondi kocha bora mwezi Februari, NBC yamjaza manoti

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!