Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Michezo Matatizo ya kifamilia yamkosesha kazi kocha Yanga
Michezo

Matatizo ya kifamilia yamkosesha kazi kocha Yanga

Dk. Mshindo Msolla, Mwenyekiti wa Yanga
Spread the love

UONGOZI wa klabu ya Yanga umeamua kuachana na aliyetaka kuwa kocha wao Cedric Kaze kutokana na kutoa taarifa ya kuchelewa kufika nchini kwa wiki tatu kutokana na matatizo ya kifamilia. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea)

Kaze ambaye ni raia wa Burundi ambapo hapo awali alishaingia makubaliano ya kukinoa kikosi hicho kwa kipindi cha miaka miwili kabla ya kupatwa na dharula.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo imeeleza kuwa, uongozi huo umeamua kutafuta kocha mwengine kutokana na Kaze kuomba kuchelewa kujiunga na klabu hiyo sababu za matatizo ya kifamilia.

Ikumbukwe Yanga inatarajia kuanza msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara tarehe 6 Septemba 2020 kwa kucheza mchezo dhidi ya Tanzania Prisons, hivyo nakuona kwao muda sio rafiki.

Pia Taarifa hiyo imeendelea kwa kueleza kuwa uongozi wa klabu hiyo umefanya kikao cha dharula na muda mchache utatangaza kocha mpya ambaye atakuja kukinoa kikosi hicho kwa msimu mpya wa mashindano.

Klabu hiyo kwa sasa inahitaji kocha kwa hali na mali kutokana na usajili mkubwa walioufanya wa wachezaji zaidi ya 10 ambao wamekuja kutia nguvu kwenye kikosi hicho ambacho tayari kimeshaanza mazoezi kuelekea kilele cha siku ya Mwanachi inayotarajia kufanyika 30 Agosti, 2020 kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Taarifa kutoka chanzo cha ndani ya klabu hiyo kimeeleza kuwa huwenda aliyekuwa kocha wao msaidizi Juma Mwambuzi atakiongoza kikosi hicho kwa muda mpaka atakapofika kocha mkuu ambaye atatangazwa hivi karibuni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Piga pesa na mechi za EUROPA leo hii

Spread the love Hatimaye Alhamisi ya EUROPA imefika ambapo leo hii mechi...

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

error: Content is protected !!