Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Michezo Yanga kujifua Zanzibar, Simba yahairisha mazoezi
Michezo

Yanga kujifua Zanzibar, Simba yahairisha mazoezi

Clifford Ndimbo, Msemaji wa TFF (kulia) akiwa na Msemaji wa Simba, Haji Manara
Spread the love

WAKATI michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa imesimama kupitisha michezo ya kimataifa ambayo ipo kwenye kalenda ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), klabu ya Yanga imeamua kwenda kisiwani Zanzibar kwa ajili ya kuweka kambi ya muda mfupi sambamba na kucheza michezo ya kirafiki. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Kikosi hicho cha Yanga kimeondoka leo asubuhi kuelekea visiwani humo na wanatarajia kucheza mchezo wao wa kirafiki hapo kesho majira ya saa 10 jioni dhidi ya timu ya Malindi FC inashiriki ligi Kuu Zanzibar.

Wakati Yanga wakifanya hivyo, uongozi wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba kupitia msemaji wao Haji Manara walitoa taarifa ya kuhairisha mazoezi ya kikosi chao ili kutoa nafasi ya kuomba dua kwa ajili ya mwekezaji mkuu wa timu yao Mohammed Dewji MO ambaye ameripotiwa kutekwa toka jana.

“Uongozi wa klabu ya Simba kwa mashauriano na Benchi la Ufundi la klabu yetu,chini ya Kocha Mkuu Patrick Aussems limeamua kuhairisha mazoezi ya Timu leo,ili kutoa fursa kwa Wachezaji na Benchi la Ufundi kushiriki ipasavyo kwenye Dua na Sala kwa ajili ya kiongozi wetu MO..tunawaomba tena na tena watanzania na wanoitakia mema nchi yetu..wasiache kumuombea uhai na uzima Bwana Mohammed Dewji..Insha’Allah kheri”

MO ambaye amekutwa na mkasa huo wa kutekwa jana alfajili kwenye Hotel ya Collesium iliyopo maeneo ya Oysterbay jijini Dar es Salaam na watu ambao bado hawajafahamika na mpaka sasa bado hajapatikana licha ya jeshi la polisi kuendelea na uchunguzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Piga pesa na mechi za EUROPA leo hii

Spread the love Hatimaye Alhamisi ya EUROPA imefika ambapo leo hii mechi...

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

error: Content is protected !!