Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Michezo Yanga, Gor Mahia ‘OUT’ Kombe la Shirikisho
Michezo

Yanga, Gor Mahia ‘OUT’ Kombe la Shirikisho

Ibrahim Ajibu, mshambuliaji wa Yanga
Spread the love

BAADA ya kumalizika kwa michezo ya kundi D, ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika hatimaye klabu za Yanga na Gor Mahia zimeaga rasmi michuano hiyo baada ya kupoteza katika michezo yao ya mwisho. Anaripoti Kelvin Mwaipungu …. (endelea).

Yanga ilipoteza mchezo wake mbele ya Rayol Sport ya Rwanda kwa kukubali kipigo cha bao moja kwa bila lililofungwa dakika 19, ya mchezo na mshambuliaji Bimenyimana baada kutumia vizuri makosa yaliyofanywa na Nahodha wa klabu hiyo Kelvin Yondani.

Kwa upande wa Gor Mahia ambayo ilikuwa ugenini mbele ya USM Alger ilikubali kipigo cha mabao mawili kwa moja, mabao ya mchezo huo kwa upande wa wenyeji yalifungwa na Price Ibara dakika ya 36 na Sayoud aliyefunga dakika ya 81 ya mchezo huku bao pekee la wakenya hao lilifungwa na Tuyisenge 83.

Kwa matokeo hayo, USM Alger ikiwa na pointi 11 kileleni, na Rayon Sports yenye pointi 9, zinafuzu hatua ya robo fainali, huku Gor Mahia ikipata alama 8, na kushika nafasi ya tatu na Klabu ya Yanga iliambulia alama nne na kushika mkia kwenye kundi hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Makala & UchambuziMichezo

TFF kuamua hatima ya Amrouche

Spread the loveHATIMA ya Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche kuendelea...

Habari za SiasaMichezo

Matinyi: Dk. Ndumbaro alifanya utani ukaguzi mechi za Yanga, Simba

Spread the loveMsemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema kauli iliyotolewa na...

Michezo

Gethsemane Group Kinondoni (GGK) waachia video ya Bwana Wastahili

Spread the loveWAIMBAJI maarufu nchini kutoka Gethsemane Group Kinondoni (GGK)SDA wameachia video...

BiasharaMichezo

Gamondi kocha bora mwezi Februari, NBC yamjaza manoti

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!