March 9, 2021

Uhuru hauna Mipaka

RC Chalamila: Tulipashwa kujipeleka polisi kufungwa

Albert Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya

Spread the love

ALBART Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya (RC) nchini Tanzania amesema, viongozi wa mkoa huo wamedhalilika kutokana na kumea kwa wizi wa dhahabu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya…(endelea).

Na kwamba, kutokana na kushindwa kusimamia madini hayo, walipaswa kujipeleka wenyewe polisi kufungwa jela walau miezi sita.

Chalamila ametoa kauli hiyo leo Jumatatu tarehe 14 Desemba 2020, mbele ya Doto Biteko, Waziri wa Madini wakati wa mkutano wake na wachimbaji wadogo wa dhahabu, wadau wa madini katika Wilaya ya Chunya.

“Tulipaswa tujipeleke wenyewe polisi walau tufungwe kwa miezi sita,” amesema Chalamila akisisitiza ni aibu na fedheha kwa mkoa huo kushuhudia wizi wa madini hayo.

Hivi karibuni, kulikuwa na sakata la utoroshaji wa madini jijini humo ambalo lilihusisha polisi wawili na wafanyabishara watatu wa madini ambao tayari wamechukuliwa hatua.

Kwenye mkutano huo, Leonard Manyesha ambaye ni Mwenyekiti wa Wachimbaji Madini Mkoa wa Mbeya amesema, sababu nyingine ya wizi wa madini kushamiri Mbeya ni kutokana na utoaji holela wa leseni.

Ameshauri, utaratibu wa utoaji leseni udhibitiwe sambamba na kufanyika utafiti wa kina kwe nye migodi ya mkoa huo.

Kutokana na hali hiyo, Rais John Magufuli wakati akimwapisha Biteko hivi karibuni, alimwagiza kufuatilia suala hilo na kuchukua hatua ili kukomesha vitendo vya utoroshaji wa madini.

error: Content is protected !!