Thursday , 18 April 2024
Home Kitengo Michezo Yajayo Yanga yanasikitisha
Michezo

Yajayo Yanga yanasikitisha

Spread the love

MPAKA sasa bado siku tano dirisha la usajili lifungwe, Yanga haijasajili mchezaji mwenye hadhi yake, ambaye angeweza kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga yenye hadhi. Anaandika Yusuf Aboud … (endelea).

Viwango vya wachezaji wapya waliosajiliwa ni vya kawaida sana, ambao kwa Yanga yenye hadhi wasingestahili kupata namba katika kikosi cha kwanza

Mrisho Ngasa, Mo Banka, Jafari Mohammed, Feisal Salum, Deus Kaseke ni wachezaji wa viwango vya kawaida na ambao Yanga tayari wapo.

Pius Buswita, Rafel Daud, Yusuph Mhilu, Ibrahim Ajib hawatofautiani sana viwango na waliosajiliwa. Hawa ni wachezaji wakusuburi benchi kwa Yanga yenye hadhi na sio kutegemewa kwenye kikosi cha kwanza.

Na ndiomaana msimu uliopita walipata nafasi baada ya wale wanaotumainiwa kupata majeraha na wengine kugoma kutokana na kutolipwa haki zao kwa wakati.

Kuna maeneo Yanga imeonyesha udhaifu wa wazi uliohitaji kuzibwa na wachezaji wapya.

Kwa mfano, Yanga inahitaji mlinda mlango mwenye kiwango cha angalau Aishi Manula au Razaq Abalola. Lakini mpaka sasa hawajasajili na hakuna dalili.

Ni bora kuwa na Mohammed Abdurahman wa JKU kuliko Youth Rostand waliyenaye.

Yanga inahitaji beki mmoja wa kati mwenye uwezo wa Vicent Bosou au Paschal Wawa wa Azam, sio huyu wa Simba. Mpaka sasa hakuna dalili za kumpata beki kama huyu.

Yanga inahitaji kiungo mmoja mchezeshaji mwenye uwezo mkubwa ambaye kwa wazawa hakuna, tukubali tusikubali mbadala wa Haruna Niyonzima pale Yanga hajapatikana.

Yanga pia inahitaji kiungo mmoja mshambuliaji anayetokea pembeni mwenye uwezo unaofanana na Shiza Kichuya, kwa upande mmoja Yusuph Mhilu akipikwa na kupewa nafasi zaidi anaweza kuziba nafasi hiyo.

Lakini pia Yanga inahitaji washambuliaji wawili wenye viwango au zaidi ya Donald Ngoma na Emanuel Okwi. Washambiaji hawa kwa wazawa hakuna.

Mpaka sasa zimebaki siku tano za usajili kufungwa, hakuna dalili za Yanga kusajili wachezaji wenye uwezo wa kuziba mapengo yaliyoonekana katika msimu uliyopita.

Wachezaji wenye sifa nilizozitaja hawapatikani hapa nchini, ni lazima watafutwe kutoka nje ya nchi.

Kwa upande mwingine wachezaji wengi wa kimataifa waliopo Yanga wameshakuwa mizigo, hawastahili kubaki Yanga.

Ni Papy Kabamba Shishimbi pekee mwenye hadhi ya kubaki Yanga, waliobaki wote wanapaswa waonyeshwe mlango wa kutokea, hawana tena uwezo na hadhi ya kubaki Yanga yenye hadhi yake, labda kwa Yanga hii iliyo hoi.

Mashabiki wa Yanga waanze kujiandaa kisaikolojia, yajayo kwao yatawatia uchungu zaidi ya haya ya sasa.

Simba, Azam, Singida United, Stand United wako vizuri zaidi msimu ujao kuliko walivyokuwa msimu uliopita.

Tusubiri!
0784 44 70 77

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

Michezo

TFF, Amrouche ngoma nzito

Spread the loveVIPENGELE vya mkataba wa kazi aliotia saini Kocha Mkuu wa...

error: Content is protected !!