Thursday , 18 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wizi mpya waibuka, TCRA wadaka 12 Mwanza
Habari Mchanganyiko

Wizi mpya waibuka, TCRA wadaka 12 Mwanza

Spread the love

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA ) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza limewatia mbaroni watu 12 wanaojihusisha na usajili wa laini za simu mtaani,kwa kujihusisha na vitendo vya utapeli kwa kusajili laini za simu kinyume na sheria. Anaripoti Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Hatua hiyo ya TCRA imekuja kufuatia malalamiko kutoka kwa wananchi ya kuwepo utapeli wa kuibiwa fedha kwenye laini zao za simu pamoja na kubadilishiwa namba za siri na watu hao wanaozunguka mtaani kusajili laini.

Watu hao, wanaopita mtaani kwa ajili ya kusajili laini za simu wakitokea katika kampuni mbalimbali za simu hapa nchini wamebainika kufanya mchezo huo hatari ka kimvuli cha kusajili laini huku wakifanya utapeli mchana.

Mkuu wa kanda ya Ziwa wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Mhandisi Francis Mihayo alisema kutokana na mchezo huo unaofanywa na watu hao wanaodiawa matapeli wa mitandao, wamepiga marufuku usajili wa simu horela mtaani bila kuwa na kibali kutoka kwa mamlaka husika.

Mhandisi Mihayo alisema wakati wanaendelea na utekelezaji wa zoezi la usajili wa laini za simu kwa njia ya Biometria ndipo imebainika kuwepo watu hao kusajili laini bila kuidhinishwa na kampuni zinazohusika.

“Watu hawa wanakiuka taratibu za usajili wa laini za simu na sasa wao kuna usajili wanaufanya wanaitwa usajili wa take away pamoja na kuwaibia wananchi pesa kwenye mitandao ya simu kwa kujifanya wanawasajilia laini za chuo.

“Leo tumeendesha oparesheni la kukamata mawakala wote wanaofanya usajili wa laini za Simu bila ya kuidhinishwa kampuni husika na kuvunja taratibu kwa kufanya mambo ambayo ni kiinyume na shera.

Mihayo alisema mtu ambaye ataruhusiwa kuendesha shughuli za usambazaji,uuzaji wa laini pamoja na kusajili ni Yule ambaye atakuwa anajihusisha na utoaji wa huduma katika fedha mtaani na sio wale wanaotembea mtaani. 

“Wale wote ambao hawana kitambulisho cha Taifa na wanataka kupata huduma ya namba mpya kutoka kwa mtoa huduma yoyote ni lazima asajiliwe kwa muda kwa kutumia kitambulisho kimoja wapo ambavyo ni leseni ya udereva, kitambulisho cha mpiga kura,kitambulisho cha mkazi Zanzimba na hati ya kusafiria,” alisema Mihayo. 

William Mnyippembe, Mhandi Mwandamizi, TCRA alisema katika mikioa ya kanda ya ziwa wameanza na mkoa wa Mwanza na kwamba tayari wamefanikiwa kuwakamata watu zaidi ya 10 katika mitaa mbalimbali ya Jiji hilo. 

“Oparesheni hii ni endelevu hivyo nawakumbusha na kuonya watu ambao wanajihusisha na shughuli hizo kuacha mara kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.

Said Ally mkazi wa mwanza ameipongeza TCRA  kwa hatua zao za kuwakamata watu hao waliokuwa wafanya vitendo vya utapeli na kuwaomba TCRA kuendelea kufanya zoezi hilo kutokana na kuibiwa mara kwa mara.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

Habari Mchanganyiko

Serikali yatoa ajira watumishi 46,000, yatangaza utaratibu mpya kuajiri

Spread the loveSERIKALI imetangaza nafasi za ajira za watumishi wa umma 46,000...

Habari Mchanganyiko

Dereva ajali iliyoua wanafunzi Arusha afikishwa kortini, aomba apelekwe rumande

Spread the loveDEREVA aliyehusika katika ajali la basi la Shule ya Msingi...

Habari Mchanganyiko

Dereva ajali iliyoua wanafunzi Arusha afikishwa kortini, aomba apelekwe rumande

Spread the love  DEREVA aliyehusika katika ajali la basi la Shule ya...

error: Content is protected !!