Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Michezo Wizara ya habari yamaliza mgogoro wa viwanja Mwenge
Michezo

Wizara ya habari yamaliza mgogoro wa viwanja Mwenge

Spread the love

WIZARA ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo imehamisha umiliki wa viwanja viwili kutoka Makonde kwenda kwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) vilivyokuwa katika eneo la Mwenge vyenye mgogoro muda mrefu baina ya wachonga vinyago na wafanyabiashara wa bidhaa hizo. Anaripoti Khalifa Abdallah … (endelea).

Waziri mwenye dhamana na Wizara hiyo Dk. Harrison Mwakyembe amesema hayo leo kutokana na mgogoro kati ya pande hizo mbili ulio dumu kwa muda wa miaka zaidi ya 30 ambapo imetoa maagizo kwa Baraza hilo baada ya kuipa umiliki.

Mwakyembe amesema kuwa Baraza hilo linatakiwa kuhakikisha wachonga vinyago na wafanya biashara wa sanaa 56 waliohamishwa kutoka katika barabara ya Bagamoyo na Sky Way Hotel na kuhamishiwa Mwenge wanapewa uwiano sawa wa kuendeleza sanaa za ufundi na soko lake.

“Wale wote walionunua vibanda kutoka kwa wahamishiwa wa mwanzo na wengine kati ya mwaka 1984 na leo BASATA ihakikishe kuwa wanahakikiwa na kueleweshwa kuwa wamenunua vibanda na si ardhi hivyo ardhi ni ya mwenyewe na watambue kuwa kuendesha biashara nyingine youote mbali ya sanaa za ufundi ndani ya viwanja hivyo ni kupoteza uhalali wao wa kuwepo hapo,” amesema.

Aidha Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Godfrey Mngereza amesema kuwa wenye biashara tofauti na Sanaa ya ufundi kwenye eneo hilo lililotengwa kwa ajili ya wachonga vinyago waondoke haraka kwakuwa agizo alilolitoa Waziri Mwakyembe ni agizo la Serikali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Piga pesa na mechi za EUROPA leo hii

Spread the love Hatimaye Alhamisi ya EUROPA imefika ambapo leo hii mechi...

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

error: Content is protected !!