Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Wizara ya Afya kudhibiti Kifua Kikuu Magereza 15
Habari Mchanganyiko

Wizara ya Afya kudhibiti Kifua Kikuu Magereza 15

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
Spread the love

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza imeanzisha kampeni ya kutokomeza ugonjwa wa Kifua Kikuu katika magereza nchini. Anaripoti Hamis Mguta … (endelea).

Hayo yamesemwa leo tarehe 5 Agosti 2019 na (CP) Owesu Ngalama, Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Jeshi la Magereza katika ufunguzi wa mafunzo kwa maofisa wa jeshi hilo uliofanyika kwenye bwalo la magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.

Cp Ngalama amesema kampeni hiyo itatekelezwa kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma, kwa kuanzisha afua ya ufuatiliaji wa kutathimini hali ya huduma za kutokomeza kifua kikuu katika magereza.

CP Ngalama amesema kuwa, afua hiyo itasaidia jeshi la magereza kuweza kubaini hali ya TB magerezani pamoja na kujua hali ya wafungwa wanaoingia magerezani.

 “Ugonjwa huu unaambukizwa kwa hewa hivyo kwa tathimini hii itasaidia kuleta utaalam mkubwa kwa wataalam wetu wa tiba waliopo kwenye jeshi kwani hali ya TB sio kubwa kwenye magereza  ila lengo ni kuhakikisha hakuna maambukizi makubwa kwani wafungwa wanaingia na kutoka,”amesema.

Aidha,ameishukuru wizara ya afya kwa kuendelea kushirikiana nao kwa muda mrefu hususan kwenye utoaji huduma za afya ikiwemo utoaji wa dawa,vifaa na vifaa tiba pamoja na masuala ya lishe kwenye vituo vya afya vilivyopo kwenye magereza.

Naye Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma (NTLP) kutoka Wizara ya Afya Dk. Beatrice Mutayoba amesema ugonjwa wa Kifua Kikuu bado ni janga.

Dk. Mutayoba ameeleza kuwa, watu takribani 27,000 hufariki dunia huku 154,000 wakikadiriwa kuugua kifua kikuu kila mwaka.

Dk. Mutayoba amesema serikali imejipanga kufikisha afua hiyo katika makundi hatarishi ikiwemo magereza,migodini,wavuvi ili kutokomeza Kifua Kikuu ifikapo mwaka 2030.

“Kama nchi tumepiga hatua kubwa sana kutokomeza ugonjwa huu hivyo tunaongeza juhudi zaidi kwenye makundi hatarishi ikiwemo ili kuwafikia kwa karibu na kuhakikisha tunapunguza maambukizi ndani ya magereza na maeneo haya”.Amesisitiza Dk. Mutayoba.

Hata hivyo, amesema mkakati wa kudhibiti kifua kikuu upo kwa wananchi wote na kwamba wanaendelea kutoa elimu kwa Watanzania wote mara waonapo dalili waende kwenye vituo vya afya kwa ajili ya vipimo, dawa, na huduma za Kifua Kikuu bila malipo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.

“Magerezani tunaweka utaratibu kwa wanaoingia kuwe na taratibu za uchunguzi ili anapokutwa na kifua kikuu waanze matibabu kwani unapoanza matibabu ndani ya wiki mbili huwezi kuambukiza wengine,”amesema Dk. Mutayoba .

Mikoa kumi na tano itakayoanza na utekelezaji  huo ni pamoja na Dar es salaam, Dodoma, Iringa, Kagera, Kilimanjaro, lindi, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Pwani, Shinyanga, Singida, Tabora na Tanga.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!