January 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wizara Katiba na Sheria wamwangukia Rais Magufuli

Mahakama ya Rufaa Tanzania

Spread the love

WIZARA ya Katiba na Sheria Tanzania, imemuomba Rais John Magufuli aongeze idadi ya majaji wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu, ili kuimarisha mfumo wa utoaji haki nchini humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Ombi hilo limetolewa leo tarehe 24 Desemba 2020 na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju, katika hafla ya kumwapisha Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji wa Mahakama ya Rufani, Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi, Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma

“Inaonesha kwamba kuna uhitaji wa kuendelea kukuomba mheshimiwa rais,  ikikupendeza utukumbuke huku kwenye mhimili wa mahakama, utuongezee nguvu tena,” amesema Mpanju na kuongeza:

“Tunahitaji katika ngazi ya Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu ili kutuongezea majaji  waweze kutusaidia katika mfumo wa utoaji haki hapa nchini.”

Rais John Magufuli

Naibu Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Katiba na Sheria, ametoa ombi hilo wakati akizungumzia uteuzi wa Jaji Mwangesi, na kwamba uteuzi huo umeacha pengo katika Mahakama ya Rufani.

“Natupa deni jingine kwako, kwenye mhimili wa mahakama kwamba akiondoka mmoja, kwa msemo wa Makamu wa Rais, Samia Suluhu pauka pakawa,” amesema Mpanju.

Akijibu ombi hilo, Rais Magufuli ameahidi kulifanyia kazi ili kuziba mapengo ya uhaba wa majaji na watumishi wengine katika sekta ya sheria.

“Nimesikia ombi la Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria,  nalifanyia kazi. Ni suala gumu lakini nafikiri, tutafika  ili kusudi tupate,” ameahidi Rais Magufuli.

error: Content is protected !!