Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yapandisha umaarufu wa Sumaye
Habari za SiasaTangulizi

Chadema yapandisha umaarufu wa Sumaye

Spread the love

HATUA ya Frederick Sumaye, aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, kutumia nembo ya taifa, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, akizungumzia mkutano wake na wahariri, imekishitua chama hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mkurugenzi wa Habari, Mambo ya Nje na Mawasiliano wa chama hicho, John Mrema, ameeleza kushutushwa kwake na hatua ya waziri mkuu huyo mstaafu, kutumia nembo ya taifa, kwa maelezo kuwa siyo jambo la kawaida.

Alisema, “kilichoishangaza ni kwamba, wito huo umeitwa kiserikali kutokana na barua yake kubebwa na nembo ya taifa.”

Hata hivyo, wakati Mrema akiendelea kushangaa matumizi ya nembo ya taifa kwa Sumaye, sheria ya viongozi wastaafu inasema, waziri mkuu mstaafu, atakuwa haki ya kuwa na ofisi binafsi; na kwamba katika ofisi hiyo, atakuwa na nembo ya taifa na bendera.

“Ofisi hii ya Waziri Mkuu Mstaafu, itakuwa na nembo ya serikali na dawati lake, litakuwa na bendera ya taifa,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi serikalini.

Alisema, “…hawa watu wanaolalamika na kushangazwa na hatua hiyo, hawafahamu sheria na wala hawasomi maandiko mbalimbali. Oktoba mwaka huu, rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, alitoa taarifa kwa vyombo vya habari na alitumia nembo ya taifa katika taarifa yake hiyo.”

Taarifa ya Kikwete ilikuwa inalengo la kutoa ufafanuzi kuhusu alichoita, “upotoshaji” uliokuwa unafanywa na baadhi ya watu, kutokana na hotuba aliyokuwa ameitoa katika kongamano la Kumbukizi ya miaka 20, ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Sumaye ameitisha mkutano na waandishi wa habari, leo tarehe 4 Desemba 2019, katika ukumbi wa mikutano wa Rubby, uliyopo katika ukumbi wa Kisenga, Kijitanyama, jijini Dar es Salaam.

Katika taarifa yake kwa umma, Sumaye amesema, mkutano wake wa leo, umelenga pamoja na mengine, “uchaguzi ndani ya chama chake.”

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na ofisi binasi ya waziri mkuu huyo mstaafu, aliyehudumu Ikulu kwa miaka 10 inasema, “mbali na kuzungumzia hali ya kisiasa, Mheshimiwa Sumaye anatarajiwa kuzungumzia uchaguzi mkuu wa viongozi wa Chadema.”

Mpaka sasa, hakuna anayefahamu hasa Sumaye anakwenda kuzungumza nini. Hata hivyo, wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema, waziri mkuu huyo amebakiza njia tatu tu:

Kuendelea na mchakato wa uenyekiti wa taifa, kuondoka Chadema; na au kujiondoa katika kinyang’anyiro hicho cha uenyekiti, lakini akabaki kuwa mwanachama wa chama hicho.

Kupatikana kwa taarifa hizo, kumekuja siku moja tangu Makamu Mwenyekiti wa chama hicho (Bara), Prof. Abdallah Safari, kukitaka chama chake, kuboresha mfumo wa demokrasia.

Prof. Safari alitoa kauli hiyo, katika mazungumzo yake na MwanaHALISI ONLINE, yaliyofanyika ofisini kwake, barabara ya Samora, jijini Dar es Salaam.

Aidha, kupatikana kwa taarifa kuwa Sumaye amepanga kukutana na waandishi wa habari, kumekuja wiki moja tangu kiongozi huyo atangaze kugombea nafasi ya mwenyekiti wa taifa wa chama hicho.

Sumaye alirejesha fomu ya kuwania uenyekiti wa Chadema, tarehe 30 Novemba 2019; fomu yake ilirejeshwa na Mustafa Muro, diwani wa Kata ya Kinondoni.

Mwanasiasa huyu alichukua maamuzi ya kurejesha fomu ya kuwania uenyekiti, siku mbili baada ya kuangushwa katika kinyang’anyiro cha uenyekiti wa Kanda ya Pwani.

Sumaye alishindwa katika uchaguzi wa mwenyekiti wa Chadema, Kanda ya Pwani, baada ya kupigiwa kura nyingi za  hapana.

Aliwaambia wajumbe wa mkutano mkuu wa Kanda ya Pwani, Alhamisi ya tarehe 28 Novemba, kwamba yuko tayari kuadhibiwa kwa kutetea haki zake ya kikatiba na kisheria.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!