Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wiki ya JPM kufanya uamuzi mgumu
Habari za SiasaTangulizi

Wiki ya JPM kufanya uamuzi mgumu

John Magufuli, Rais wa Tanzania
Spread the love

RAIS John Magufuli anafikiria kufungua Vyuo Vikuu wiki ijayo, ili wanafunzi wanendelee na masomo iwapo maambukizi ya virusi vya corona yataendelea kupungua. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam…(endelea)

Akizungumza katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ushirika wa Chato leo tarehe 17 Mei 2020, alipokwenda kufanya ibada na mkewe mama Janeth amesema, anafikiria michezo irejee katika wiki inayoanza kesho na kwamba bado ‘anasikilizia’.

“Mungu ashukuruwe sana kwa kutusikiliza, kwa mwendo huu nataka niendelee kusisitiza tuchukue tahadhari, tuendelee kumuomba.

 “…na kwa trend (mwenendo) wiki inayoanza nimepanga kufungua vyuo ili wanafunzi wetu waendelee na masomo, nimepanga pia sisi kama taifa michezo iendelee kwa sababu michezo ni sehemu ya burudani kwa Watanzani,” amesema Rais Magufuli.

 Kwa mara ya kwanza, mtu aliyeambukizwa virusi vya corona alitangazwa tarehe 16 Machi 2020.

 Hata hivyo, Rais Magufuli ametoa orodha na vituo vya afya vilivyohudumia watu walioambukizwa virusi hivyo na idadi ya wagnjwa waliosalia kwa sasa.

Baadhi ya vituo hivyo na idadi ya wagonjwa ni Hospitali ya Amani ambayo ilikuwa na wagonjwa 198, sasa wamebaki 12; Mloganzila ilikuwa ina wagonjwa 30, sasa wamebaki sita; Kibaha (Lulanzi) walikuwa zaidi ya 50, sasa wapo 22; Hospitali ya Agha Khan wamebaki 31.

 Amesema Hospitali ya Hindu Mandala wamebaki 16, Regency (17), TMJ (7), Rabinisia Tegeta (14).

 “Kwa hiyo, mnaweza kuona trend (mwenenndo) ya majibu ya bwana Mungu wetu yalivyofanya kazi, lakini hata katika mikoa Arusha, wana vituo vitatu; Mshono (11), Longido hakina mgonjwa hata mmoja, Karatu  kuna kituo kinaitwa  Dofu, hakina mgonjwa,” amesema.

 Pia amesema, Mwanza ambapo kuna vituo 10, vinane vilivyopo Busweru vina wagonjwa wawili, Misungwi kuna wagonjwa wawili na kwamba wote wanahali vizuri.

 Rais Magufuli amesema, viyuo vya Ukerewe Nyakatungulu, Magu John Mongela, Kituo cha Mkuyuni, Buchosa Nyangunge na Sengerema havina wagonjwa na kuwa, Hospitali Kuu mbili Bungando na  Seketure kuna wagonjwa wawili.

 Amesema, ugonjwa huu ni kama yalivyo magonjwa mengine na ndio sababu hajasukumwa kuifunga nchi, kwa kuwa tayari nchi zingine zimeingia kwenye matatizo kutokana na uamuzi wa kuwaweka wananchi wake ndani.

 “Sitaki kueleza matatizo wanyoyapata katika maeneo mengine, nyinyi wenyewe mnajua lakini sisi tumeamua kwenda hivi. Tumeamua tumtangulize Mungu, tulianza na mungu na tutamaliza na Mungu,” amesema.

Amewataka Watanzania kutoa hofu kwa kuwa, kuna maneno mengi yaliyotiwa chumvi, kwamba hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko corona yenyewe.

 “Inawezekana watu wamepoteza maisha kwa sababu ya hofu au kudanganywa, yupo rafiki yangu mmoja injinia, nataka tutoe mfano wa kweli.

 “Alipata kiharusi, akabebwa akapelekwa Muhimbili, akakaa pale siku mbili tatu kwamba huyu ana corona, akapelekwa Amana akalazwa, watu wanamuogopa ana corona.

 “Baadaye ndugu zake wakaona kama amecheleweshwa hivi, ngoja tumchukue wakampeleka kwenye Hospital Agha Khan, na kule kwasababu aliambiwa ana corona, wakamuweka kwenye chumba maalumu wakawaambia watoe advance (watangulize) milioni sita.

 “Wakamchukua vipimo walivyoenda kumpima, wakakuta hana corona, ndipo wakamuhamisha kwenye hodi ya kawaida, sasa ameshapona na yupo nyumbani anazungumza,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!