ILI kutumiza lengo la afya kwa wote, shirika la afya ulimwenguni (WHO) limeanzisha mpango wa kujenga vituo vya kuratibu matukio ya sumu katika sehemu ambazo zina uwezo wa kuchunguza na kutambua sumu kwa lengo la kuijengea jamii uwezo wa kuwa salama. Anaandika Eunice Laurian … (endelea)
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam mratibu mkuu wa kituo kipya cha kuratibu matukio ya sumu nchini, Dk Yohana Goshashy amesema mpango huo ulipelekea uanzishwaji wa vituo vingine vya kuratibu matukio ya sumu Afrika ,serikali kupitia wizara ya afya na ustawi wa jamii wakati huo ilipendekeza kituo kianzishwe katika maabara ya mkemia mkuu wa serikali.
Amesema sababu ya kuwepo kwa kituo cha kuratibu matukio ya sumu katika maabara ya mkemia mkuu wa serikali ni kutokana na madhara mengi ya sumu husababishwa na sumu zina asili ya kemikali, ni maabara yenye uwezo wa kuchunguza na kugundua aina mbalimbali za kemikali na sumu.
Ameongeza kuwa kituo hicho kitakuwa kinafanya kazi ya uhuduma ya utoaji wa taarifa za matukio ya sumu,kuzuia ajari za kemikali na kuratibu matukio ya sumu, kufanya tafiti mbalimbali zinanasohusu sumu, kukusanya kumbumbuku za matukio ya sumu na kutengeneza kanzi data na nakutoa ushauri na jinsi ya kutoa bita kwa wagonjwa walioathiriwa na matukio ya sumu.
Serikali kupitia Wizara ya afya na ustawi wa jamii wakati huu ilipendekeza kituo kianzishwe katika maabara ya Mkemia Mkuu wa serikali maabara hiyo iliendeleza jitiahada zilizochukua miaka kadhaa na hatimaye mwaka 2014 kituo cha kuratibu matukio ya sumu nchini (NPCC) kilizinduliwa na Mhe. Waziri wa afya na Ustawi wa jamii.