Thursday , 25 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu WhatsApp yatumika udanganyifu wa mitihani, 65 mbaroni
ElimuHabari MchanganyikoTangulizi

WhatsApp yatumika udanganyifu wa mitihani, 65 mbaroni

Whatsapp
Spread the love

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Kagera, inawashikilia wanafunzi 38 wa Chuo cha Ufundi (VETA) Wilaya ya Bukoba mkoani humo na wakufunzi wao wawili kwa tuhuma za kufanya udanganyifu katika mitihani. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Wakufunzi hao ni; Francis Mwangosi na Ssenabulya Daud pamoja na Mkuu wa chuo hicho, Baluhi Mitinje waotuhumiwa kutumia vibaya ofisi.

Pia, Takukuru inawashilia wanafunzi 21 wa Chuo cha Tuinuane VTC na wakufunzi wao wawili pamoja na mkuu wa chuo hicho kutokana na tuhuma kama hizo za VETA.

Taarifa iliyotolewa jana Jumanne tarehe 15 Desemba 2020 na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kagera, John Joseph akielezea udanganyifu huo uliohusisha siku za mikononi walizoingianazo kwenye vyumba vya mitihani na kutumia makundi ya WhtsApp kufanya udanganyifu.

Mbali na kuwashikilia wanafunzi na wakufunzi hao, Joseph amesema, walikamata jumla ya simu 41, kati ya hizo, 38 ni za wanafunzi na tatu za wakufunzi ambazo wanafunzi waliokuwa wameingia nazo katika chumba cha mtihani wa Taifa wa elimu ya ufundi.

Brigedia Jenerali, John Mbungo, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru

“Simu hizi zilikuwa zinatumiwa na wanafunzi waliokuwa katika chumba cha mtihani kurusha maswali kwa wakufunzi ambao walikuwa ofisini kwao, waliyajibu maswali hayo na kisha kuwatumia wanafunzi majibu husika wakiwa ndani ya chumba cha mtihani,” alisema Joseph.

Joseph alisema, mbali na wanafunzi hao 38 kuwashikilia, taasisi hiyo inawashikilia wanafunzi wengine 21 wa Chuo cha Tuinuane VTC pamoja na wakufunzi wao wawili, Charles Byabachwezi na Verdiana Myaka pamoja na Mkuu wa chuo hicho, Emmanuel Jonas.

Chuo cha Tuinuane kipo Kijiji cha Kabale Kata ya Karabagaine pamoja na wasimamizi wawili wa mitihani ambao ni waajiriwa wa Chuo cha Ufundi-Veta Mkoa wa Kagera.

Hii ina maana kwamba, ukijumlisha wote wanaoshikiliwa ni 65.

Joseph alisema, wanafunzi Tuinuane nao wanatuhumiwa kuingia na simu katika chumba cha mtihani na kisha kutumia simu hizo kupiga picha maswali na kuyarusha kwa wakufunzi waliokuwa nje ya chumba cha mtihani ili kuwapatia majibu ya maswali hayo kwa njia ya makundi ya WhatsApp yaliyotengenezwa na wakufunzi na ndio wasimamizi wa makundi hayo.

Alisema, katika Chuo cha Tuinuane ambacho pia kimesajiliwa na VETA, licha ya kukamata wanafunzi 21, wamekamata pia simu 21 za wanafunzi na simu nne za wakufunzi pamoja na fedha SH.151,000 ambazo zilikuwa zimechangwa na wanafunzi kwa ajili ya kuwapatia wasimamizi wa mitihani hiyo ya taifa.

“Wanafunzi na wakufunzi tajwa, wanashikiliwa kufuatia taarifa za kiintelejensia zilizobainishwa na Takukuru Mkoa wa Kagera kuwa kumekuwapo na udanganyifu katika mitihani ya taifa ya elimu ya ufundi katika chuo cha Tuinuane VTC na Veta mkoani Kagare,” amesema Joseph

“Uchunguzi unaoendelea umebaini kuwepo kwa ukiukwaji mkubwa wa taratibu za mtihani katika Chuo cha Veta mkoani Kagera pamoja na Chuo cha Tuinuane VTC kunakofanywa na wakuu wa vyuo hivyo kwa kushirikiana na baadhi ya wakufunzi, wanafunzi pamoja na wasimamizi wa mitihani.”

“Lengo likiwa ni kuwasaidia wanafunzi wao na kutaka kuonyesha kuwa vyuo hivyo vinafanya vizuri,” alisema Joseph.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

error: Content is protected !!