Wema Sepetu (kulia) akitoka na mama yake mahakamani Kisutu
Wema Sepetu (kulia) akitoka na mama yake mahakamani Kisutu

Wema Sepetu azidi kusota mahakamani

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imehailisha usikilizwaji wa kesi  ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili msanii wa Filamu nchini Wema Sepetu mpaka Novemba 24, mwaka huu, anaandika Faki Sosi.

Kesi hiyo ipo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba ambapo leo upande wa Jamhuri ulidai kuwa utafika mahakamani hapo na mashahidi wawili.

Wema  alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Februari 22, mwaka huu pamoja na Matilda Abass na Angelina Msigwa waliotajwa kuwa ni wafanyakazi wake wa ndani na kusomewa shitaka moja la utumiaji dawa ya kulevya aina ya bangi. Alikana shitaka.

Awali Oktoba 31, mwaka huu, mahakama hiyo ilitoa uamuzi wa mapingamizi yaliyowasilishwa na wakili wa utetezi Peter Kibatala wa kupinga hati ya ukamataji mali iliyowasilishwa mahakamani hapo na upande wa mashtaka.

Hakimu Simba alipokea hati hiyo ya baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili na kuingiza kwenye rekodi za mahakama hiyo.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imehailisha usikilizwaji wa kesi  ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili msanii wa Filamu nchini Wema Sepetu mpaka Novemba 24, mwaka huu, anaandika Faki Sosi. Kesi hiyo ipo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba ambapo leo upande wa Jamhuri ulidai kuwa utafika mahakamani hapo na mashahidi wawili. Wema  alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Februari 22, mwaka huu pamoja na Matilda Abass na Angelina Msigwa waliotajwa kuwa ni wafanyakazi wake wa ndani na kusomewa shitaka moja la utumiaji dawa ya kulevya aina ya bangi. Alikana shitaka. Awali Oktoba 31, mwaka huu,…

Review Overview

User Rating: Be the first one !
0

About Faki Sosi

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube