Wema Sepetu afikishwa mahakamani Kisutu

WEMA Sepetu, Miss Tanzania mwaka 2006 na mwigizaji wa filamu Tanzania, amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Alhamisi Novemba Mosi, 2018. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Pamoja na Wema kufikishwa mahakamani hapo saa 4 asubuhi na kupelekwa katika chumba cha mahabusu, lakini bado haijajulikana atashitakiwa kwa kosa gani.

Msanii huyo alitinga mahakamani hapo akiwa ameambatana na polisi kike, akiwa amevaa miwani na kujitanda ushungi kwa lengo la kujificha.

Kufikishwa mahakamani kwa Wema kunatokana na taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii juu ya kukamatwa kwa msanii huyo.

WEMA Sepetu, Miss Tanzania mwaka 2006 na mwigizaji wa filamu Tanzania, amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Alhamisi Novemba Mosi, 2018. Anaripoti Mwandishi Wetu ... (endelea). Pamoja na Wema kufikishwa mahakamani hapo saa 4 asubuhi na kupelekwa katika chumba cha mahabusu, lakini bado haijajulikana atashitakiwa kwa kosa gani. Msanii huyo alitinga mahakamani hapo akiwa ameambatana na polisi kike, akiwa amevaa miwani na kujitanda ushungi kwa lengo la kujificha. Kufikishwa mahakamani kwa Wema kunatokana na taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii juu ya kukamatwa kwa msanii huyo.

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

error: Content is protected !!
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On YoutubeVisit Us On Instagram