Wema afikishwa mahakamani, aachiwa kwa dhamana – MwanaHALISI Online
Wema Sepetu akiwasili kituo cha Polisi cha Kati
Wema Sepetu akiwasili kituo cha Polisi cha Kati

Wema afikishwa mahakamani, aachiwa kwa dhamana

WEMA Sepetu na wenzake wawili wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo na kusomewa mashitaka matatu yanayohusiana na matumizi ya dawa za kulevya aina ya bangi, anaaandika Mwandishi Wetu.

Akisomewa mashtaka na wakili wa serikali Nassoro Katuga mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba imeelezwa kuwa msanii huyo alikutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya aina ya bangi.

Wakili Nassoro Katuga amesema mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa Wema Sepetu mnamo Februari 4, 2017 katika eneo la Kunduchi Ununio watuhumiwa watatu akiwemo Wema walitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha sheria ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya kifungu cha 17 (1) (a) cha makosa hayo.

Msanii huyo na wenzake wameachiwa kwa dhamana ya Sh. milioni tano na wadhamini wawili na kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 22, 2017 itakapotajwa tena na kwamba bado uchunguzi unaendelea.

About Mwandishi Wetu

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube