JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limeeleza kuwa, linawashilikia watu watatu wanaoshukiwa kuhusika na tukio la kutekwa kwa Mfanyabiashara Mohammed Dewji, lililotokea alfajiri ya leo tarehe 11 Oktoba 2018, katika Gym ya hoteli ya Colosseum iliyoko Oysterbay jijini Dar es salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, amewaambia wanahabari kuwa, MO Dewji anayedaiwa kutekwa kimafia, alitekwa na wazungu wawili waliokuwa na silaha za moto.
Kamanda Mambosasa ameeleza kuwa, wazungu hao wawili waliwasilia hotelini hapo wakiwa na gari binafsi aina ya Surf ambalo walilipaki karibu na gari ya MO Dewji, kisha kumchomo mfanyabiashara huyo ndani ya gari lake na kumpakia kwenye gari lao, na kuondoka naye kusikojulikana.
Kwa mujibu wa taarifa za awali zilizo tolewa na mashuhuda wa tukio hilo, inasemekana watu hao walikuwa wanne huku wakiwa wamefunika nyuso zao ‘Ninja’, walifyatua risasi hewani kuwatishia watu waliokuwa karibu na eneo hilo kabla ya kuondoka naye.
Leave a comment