Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Waziri wa tatu afariki kwa corona Zimbambwe
Kimataifa

Waziri wa tatu afariki kwa corona Zimbambwe

Joel Biggie Matiza, aliyekuwa Waziri wa Usafirishaji wa Zimbabwe
Spread the love

 

WAZIRI wa Usafirishaji wa Zimbabwe, Joel Biggie Matiza, amefariki dunia jana Ijumaa tarehe 22 Januari 2021, katika Hospitali ya St. Anne Harare nchini humo, alipokuwa anatibiwa maambukizo ya virusi vya corona (COVID-19). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Matiza anakuwa waziri watatu wa Zimbambwe kufikwa na mauti kwa corona ndani ya wiki moja iliyopita.

Tarehe 20 Januari 2021, Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara, Dk. Sibusiso Moyo (58), alifariki dunia katika moja ya hospitali nchini humo alipokuwa akitibiwa maambukizo ya corona.

Dk. Sibusiso Moyo, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Zimbabwe

Waziri mwingine aliyefariki kwa corona ndani ya wiki moja ni Ellen Gwaradzimba ambaye ni waziri wa nchi, anayeshughulikia masuala ya mikoa aliyefariki tarehe 15 Januari 2021.

Pia, Morton Malianga (90), aliyewahi kuwa naibu waziri wa fedha, alifariki dunia tarehe 15 Januari 2021.

Ellen Gwaradzimba, aliyekuwa Waziri wa Nchi wa Zimbabwe

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!