Tuesday , 19 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Waziri wa JPM abanwa bungeni
Habari za SiasaTangulizi

Waziri wa JPM abanwa bungeni

Dk. Philip Mpango
Spread the love

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Phillip Mpango ametakiwa kutoa idadi ya wananchi waliotolewa kwenye unyonge wa umasikini, tangu serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akichangia hoja leo tarehe 7 Novemba 2018 bungeni jijini Dodoma, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche amehoji kuwa, tangu serikali ya Rais John Magufuli ilipoingia madarakani ilikuta idadi ya wanyonge wangapi na walioondolowe kwenye unyonge huo ni wangapi.

Katika hatua nyingine, Heche amehoji mahali zilipo fedha zilizokusanywa na serikali ikiwa baadhi ya wananchi wanalia fedha hazionekani mitaan, i huku serikali ikijinasibu kwamba inakusanya fedha nyingi.

Wakati akichangia hoja kuhusu mapendekezo ya mpango wa taifa wa maendeleo wa mwaka 2019/20, Heche ameeleza kwamba, serikali imeshindwa kutekeleza mpango wake wa kupelekea fedha za maendeleo kwa mwaka wa fedha wa 2017/18 ambapo ilipeleka Sh.6 trilioni badala ya Sh. 12 trilioni ilizopanga kupeleka.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Zanzibar mbioni kuanza uchimbaji mafuta na gesi baharini

Spread the loveSERIKALI ya Zanzibar, imekamilisha mchakato wa uchimbaji wa mafuta na...

Habari za Siasa

Wizara ya afya yataja mafanikio 10 miaka mitatu Samia madarakani

Spread the loveWIZARA ya Afya imetaja mafanikio 10 iliyoyapata ndani ya miaka...

Habari za Siasa

Mbozi walilia kuwa manispaa, majimbo 3

Spread the loveHALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imeeleza dhamira yake...

Habari za Siasa

Wabunge waitaka TPDC kuongeza kasi ya kuunganisha wateja gesi asilia

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini...

error: Content is protected !!