Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Waziri wa fedha atoa onyo, Watanzania wakiongezeka
Habari za SiasaTangulizi

Waziri wa fedha atoa onyo, Watanzania wakiongezeka

Dk. Philip Mpango
Spread the love

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, ametoa onyo kwa mashirika mbalimbali kutotoa taarifa za makadirio ya takwimu za Watanzania na kuzichapisha bila ya kushirikisha ofisi ya Taifa ya Takwimu na kuhatalisha maendeleo ya nchi yetu, serikali itawachukulia hatua za kisheria. Anaripoti Angel Willium … (endelea).

Mpango ametoa onyo hilo wakati wa uzinduzi wa Takwimu ya makisio ya idadi ya watu nchini ambapo sasa Tanzania inakisiwa kuwa na watu 54.2 milioni, kwa upande wa Tanzania Bara kuna watu 52.6 milioni na Zanzibar watu 1.6 milioni kwa makisio ya mwaka huu.

Takwimu hizo zinaonesha itakapofikia mwaka 2121 Tanzania itakuwa na makadirio ya watu 59.4 milioni na itakapofika mwaka 2030 itafikia idadi ya watu 77.5 milioni wakati nchi zote zitakuwa zinatathimini mafanikio na changamoto za malengo ya mpango wa Dunia wa maendeleo endelevu.

Waziri Mpango amesema, hairuhusiwi kufanya takwimu kiholela kwani ni kosa kwa mujibu wa sheria namba 9 ya 2015, hivyo wadau wa takwimu wa ndani na nje ya nchi wanatakiwa kutumia takwimu zilizozinduliwa leo ambazo ndiyo sahihi.

“Makadirio ambayo hayaendani na idadi sahihi ya watu yanahatarisha maendeleo. Kapo kashirika kamoja hivi karibuni kametoa taarifa za ajabu. Tunamfutilia tutapambana naye tu,” amesema Mpango.

Mpango amesema, kasi ya ongezeko ya idadi ya watu inaleta changamoto kubwa kwa serikali kwani katika takwimu ya mwaka huu inaonyesha kuwa asilimia 50 ni watoto wenye umri wa chini ya miaka 18 hivyo ni changamoto kwa maendeleo ya nchi yetu, kwani kundi hilo lina mahitaji ya kipekee ambayo lazima yatimizwe na serikali.

Aidha Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taarifa ya Takwimu Albina Chuwa amesema makadirio yaliyozinduliwa na Waziri Mpango yanaonesha kuwa umri wa kuishi kwa mtanzania atakaezaliwa leo ni miaka 65 ikilinganishwa na miaka 61 ya mwaka 2012.

Chuwa amesema kipindi cha miaka mitano maisha ya mtanzania yameendela kuboreka zaidi hususani sekta ya afya na zinazohusu jamii na uchumi, vifo vya watoto wachanga makadirio yanaonesha kiwango hiki kinaendelea kupungua kutoka 43 kwa kila watoto 1000 wanaozaliwa hai hadi kufikia 33 mwaka 2018.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!