Thursday , 25 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Waziri Ummy atoa darasa la unyonyeshaji watoto
Afya

Waziri Ummy atoa darasa la unyonyeshaji watoto

Spread the love

ULISHAJI wa mtoto usio sahihi unaochangiwa na mama kuelemewa na majukumu mengi ya kazi hivyo kukosa muda wa kutosha wa kumtunza mtoto ni sababu kubwa ya utapiamlo kwa watoto. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamesema leo Jumamosi tarehe 1 Agosti 2020 na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa Tanzania, Ummy Mwalimu wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji ambayo kitaifa yamefanyika wilayani Muheza Mkoa wa Tanga.

“Ni dhahiri mchango wa mwanamke katika familia, ajira na uzalishaji kwa ujumla ni mkubwa, ni muhimu kuwatia moyo na kuwasaidia wanawake ili waweze kufanya majukumu ya uzalishaji na utunzaji familia kwa ukamilifu,” amesema Ummy.

Waziri Ummy amesema, jamii ina wajibu wa kuwawezesha wazazi, hususani wanawake waweze kunyonyesha watoto wao maziwa ya mama pekee kwa miezi sita ya mwanzo baada ya kujifungua.

Aidha, amesema, watoto wanapotimiza miezi sita waanzishiwe vyakula vya nyongeza vyenye ubora kilishe huku wakiendelea kunyonyeshwa hadi watakapotimiza umri wa miaka miwili.

Takwimu za hali ya ulishaji watoto nchini Tanzania zinaonesha, takribani asilimia 97 ya watoto wenye umri chini ya miaka miwili wananyonyeshwa maziwa ya mama, idadi ya watoto wanaoanzishiwa kunyonyeshwa maziwa ya mama kwa wakati sahihi katika kipindi kisichozidi saa moja baada ya kuzaliwa ni asilimia 53.

Idadi ya watoto wanaonyonyeshwa maziwa ya mama pekee bila kupewa maji, vinywaji na vyakula vingine katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo baada ya kuzaliwa ni asilimia 58.

Waziri Ummy amesma, idadi ya watoto wanaoanzishiwa vyakula vya nyongeza kwa wakati sahihi katika umri wa miezi 6 hadi 8 ni asilimia 87 na idadi ya watoto wenye umri wa miezi 6 – 23 wanaolishwa chakula kinachokidhi vigezo vya ubora kilishe ni asilimia 35.

“Vigezo hivyo ni idadi sahihi ya milo anayopewa mtoto kwa siku kulingana na umri wake na mlo uwe na mchanganyiko wa vyakula kutoka kwenye makundi yasiyopungua manne ya vyakula,” amesisitiza.

Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani kwa mwaka 2020 yamebebwa na kauli mbiu inayosema “Tuwawezeshe wanawake kunyonyesha watoto kwa afya bora na ulinzi wa mazingira.”

Amesema kauli mbiu hii inalenga kukumbusha mchango wa unyonyeshaji katika utunzaji wa mazingira ya dunia na ikolojia yake sanjari na kulinda afya ya binamu.
Amesema kauli mbiu hii inahimiza jamii kuboresha kasi ya unyonyeshaji sanjari na kupunguza kiwango cha matumizi ya maziwa na vyakula mbadala vya watoto wachanga na wadogo.

“Aidha, tukumbuke matumizi ya maziwa na vyakula mbadala vya watoto wachanga na wadogo yanakwenda sanjari na matumizi ya vifungashio mbalimbali vikiwemo vya plastiki, nishati ikiwemo kuni na mkaa, maji, chupa za kulishia watoto na ongezeko la hewa ya ukaa inayoathiri mazingira ya dunia,” amesema Waziri Ummy.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!