Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Waziri Ummy aonya wavuta sigara hadharani, atoa maagizo
Habari Mchanganyiko

Waziri Ummy aonya wavuta sigara hadharani, atoa maagizo

Ummy Mwalimu, Waziri wa TAMISEMI,
Spread the love

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema Tanzania kama nchi nyingine za Kiafrika wavutaji wa tumbaku wako hatarini kuyumba kiuchumi na kupata magonjwa yasiyoambukizwa ikiwa tahadhari hazitachukuliwa mapema. Anaandika Hamis Mguta…(endelea).

Waziri Ummy amesema hayo leo tarehe 4 Juni 2020 wakati wa uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa matumizi ya tumbaku kwa watu wazima ya mwaka 2018 nchini uliofanyika katika ukumbi wa Takwimu jijini Dodoma.

Amesema utafiti huo umeonesha kwa wastani, matumizi ya tumbaku kwa mtu mmoja kwa mwezi inagharimu Sh.28,840 fedha ambayo ingetosha kupunguza kiwango cha umaskini wa mahitaji ya msingi kwa mtu mmoja mmoja kwa mwezi kwa asilimia 58 na umaskini wa kupindukia (mahitaji ya chakula) kwa mtu mmoja mmoja kwa mwezi kwa asilimia 85.

 

“Kwa kutumia taarifa za Matokeo ya Viashiria Muhimu vya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya binafsi kwa Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18, fedha za kujikimu kwa ajili ya mahitaji ya msingi kwa mwezi kwa mtu mmoja ni Sh.49,320 na mahitaji ya chakula kwa mwezi kwa mtu mmoja ni Sh. 33,748,” amesema Waziri Ummy.

Kwa mujibu wa utafiti huo, matokeo yameonesha mtu mmoja kati ya 10  (8.7%), wenye umri wa miaka 15 au zaidi nchini Tanzania wanatumia tumbaku ya aina yeyote hivyo kuwa na watu milioni 2.6 kati ya watu zaidi ya  milioni 55. Wanaume ni asilimia 14.6 na wanawake ni asilimia 3.2.

Aidha, Waziri Ummy amesema watu 4 kati ya 10 (40.3%) nchini wamewahi kuona onyo la matumizi ya tumbaku kupitia redio au runinga.

Pia, matokeo ya utafiti yameonesha, watu 9 kati ya 10 (92.3%) wenye umri wa miaka 15 au zaidi, wanaamini uvutaji wa sigara husababisha magonjwa, wakati watu 8 kati ya 10 (84.4%) wanaamini kuvuta hewa ya mtu anaevuta sigara kunaweza kuwasababishia magonjwa hata kama wao hawavuti sigara.

Katika kipindi cha miezi 12 iliyopita.  Taarifa inaonesha watu 4 kati ya 10 (32.9%) wameathiriwa na moshi wa tumbaku sehemu za kazi ikiongozwa na sehemu za mabaa na kumbi za starehe kwa asilimia 77 (watu milioni 3), maeneo ya huduma za biashara za vyakula asilimia 31.1(watu milioni 3.5) na majumbani asilimia 13.8 (watu milioni 4.1).

Waziri Ummy amesema, utafiti huo una umuhimu wa kipekee katika wizara, kwani matokeo yake yatasaidia katika kutathmini hatua zilizofikiwa katika kupambana na magonjwa makuu manne yasiyoambukiza ambayo ni saratani, magonjwa ya moyo, magonjwa ya mfumo wa hewa na kisukari.

Katika kuhakikisha elimu dhidi ya athari ya tumbaku inaifikia jamii ipasavyo, Waziri Ummy ametoa maelekezo kwa  watendaji wa wizara hiyo kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu na wadau wengine, kutengeneza au kupitia upya Sheria ya kudhibiti matumizi ya Tumbaku ili iendane na Mkataba wa Kimataifa wa kudhibiti matumizi ya Tumbaku.

Pia, amesema, kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu madhara yake; wizara ya elimu kuendelea kuimarisha juhudi za kuwakinga wanafunzi dhidi ya tumbaku na bidhaa zake; wizara ya mambo ya ndani kuhakikisha wale wanaokiuka miongozo kama vile kuendelea kuvuta sigara kwenye maeneo ya wazi wanachukuliwa hatua stahiki.

Amesema, watengenezaji na wauzaji wa sigara, kufuata miongozo iliyowekwa na Serikali ikiwemo kutokuweka mabango au kutangaza na kuhamasisha matumizi ya sigara, kupitia bidhaa kama miamvuli, T-Shirts, kofia, na kutowauzia watoto wenye umri chini ya miaka 18; jamii kuacha kutumia tumbaku na bidhaa zake na Taasisi za Utafiti kufanya Tafiti za kuangalia vifo vitokanavyo na matumizi ya tumbaku ilikuwe na takwimu za nchi na siyo kutegemea za kutoka nje.

1 Comment

  • Heko Waziri kwa maneno murwa. Naomba sasa vitendo. Piga marufuku matangazo au kampeni zote za sigara. Marufuku kwa watoto chini ya 18 kuvuta au kuuza sigara. Kila paketi iwe na onyo kwa herufi kubwa “SIGARA INAUA”. Kodi juu ya sigara iongezwe kwa asilimia 100. Ni kufidia gharama za kuwatibu wagonjwa wa saratani ya sigara pale Ocean Road
    Maneno mengi yamesemwa dhidi ya sigara. Sasa vitendo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!