Madereva wa malori wa Tanzania waliokwama katika mpaka wa Tanzania na Kenya uliopo Namanga

Waziri Tanzania awapa pole madereva waliokwama Namanga 

Spread the love

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto nchini Tanzania, Dk. Godwin Mollel amefanya ziara katika mpaka wa Tanzania na Kenya Namanga jijini Arusha na kuzungumza na madereva wa malori yanayokwenda Kenya ili kusikiliza changamoto zinazowakumba. Anaripoti Mwandishi Wetu, Namanga … (endelea).

Dk. Mollel amefanya ziara hiyo leo Jumatano tarehe 10 Juni 2020, ikiwa ni sehemu ya kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakumba madereva hao, katika kipindi hiki ambacho Dunia imekumbwa na maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19).

Dk. Mollel amesema, Serikali imeliona tatizo hilo na kuweka wazi itaongeza kasi katika kuhakikisha inapata suluhu ya changamoto wanazokumbana nazo madereva hao katika eneo la mpaka wa Namanga. 

“Nimekuja kuwaambia poleni, lakini Serikali yetu itaenda kwa kasi ya ajabu kuhakikisha kwamba hili tatizo lenu katika mpaka huu linatatuliwa,” amesema.

Aidha, Dk. Mollel amewataka madereva hao kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho, Serikali inatafuta utatuzi wa changamoto yao, huku akiwapa salamu kutoka kwa Rais wa Tanzaniam, Dk. John Magufuli na kusema anawapenda sana.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto nchini Tanzania, Dk. Godwin Mollel

Mbali na hayo Dk. Mollel amesema kuwa changamoto hii iliyojitokeza katika mpaka wa Namanga ni suala mtambuka ambalo linahusisha Wizara zaidi ya moja, huku akiweka wazi suala hilo lina uhusiano wa kibiashara na uchumi baina ya nchi hizo.

Naye, dereva wa malori yanayokwenda nchini Kenya, Abdullah Hassan amesema, kama madereva hawakubaliani na majibu ya vipimo wanavyopewa kutoka Kenya kutokana na vipimo hivyo kuonesha idadi kubwa ya madereva kuwa na ugonjwa wa corona jambo ambalo sio kweli.

“Tunaishi maisha magumu sana kutokana na hali iliyojitokeza, na kunachosikitisha zaidi, sisi hatukubaliani na vipimo ambavyo tunapimwa upande wa pili,” amesema

Kwa upande wake, Japhet Jeremiah alisema, wamekuwa wakiombwa kiasi cha Sh. 2000 za Kenya ili kuandikiwa kuwa hawana corona, hali aliyeweka wazi kuwa ni uonevu kwa madereva kutoka Tanzania.

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto nchini Tanzania, Dk. Godwin Mollel amefanya ziara katika mpaka wa Tanzania na Kenya Namanga jijini Arusha na kuzungumza na madereva wa malori yanayokwenda Kenya ili kusikiliza changamoto zinazowakumba. Anaripoti Mwandishi Wetu, Namanga ... (endelea). Dk. Mollel amefanya ziara hiyo leo Jumatano tarehe 10 Juni 2020, ikiwa ni sehemu ya kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakumba madereva hao, katika kipindi hiki ambacho Dunia imekumbwa na maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19). Dk. Mollel amesema, Serikali imeliona tatizo hilo na kuweka wazi itaongeza kasi katika kuhakikisha…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!